Nenda kwa yaliyomo

Kukuziwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fulica)
Kukuziwa
Kukuziwa wa kawaida
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Gruiformes (Ndege kama korongo)
Familia: Rallidae (Ndege walio na mnasaba na viluwiri)
Ngazi za chini

Jenasi 4 za kukuziwa:

Kukuziwa ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Rallidae. Wana mnasaba na viluwiri lakini ni ndege wa maji wa kweli (tazama shaunge pia). Wanaachana na viluwiri kwa kuwa na kigao kidogo juu ya domo. Rangi yao ni nyeusi au kijivu nzitu na mabawa ya spishi nyingi yana rangi ya kahawa. Rangi ya domo na kigao ni nyeupe au nyekundu. Vidole vyao vina ndewe, siyo ngozi kama mabata, ili kusogeza mbele kwa urahisi majini. Hula mimea, wanyama wadogo na mayai. Hujenga tago kubwa kwa mimea majini au ardhini na huyataga mayai 6-12.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia

[hariri | hariri chanzo]
  • Fulica chathamensis (Chatham Island Coot) (mwisho wa Quaternary)
  • Fulica infelix (Juntura, MMA, mwanzo wa Pliocene)
  • Fulica prisca (New Zealand Coot) (mwisho wa Quaternary)
  • Fulica shufeldti (Amerika ya Kaskazini, Pleistocene) – labda spishi ndogo ya Fulica americana
  • Gallinula balcanica (Varshets, Bulgaria, kati ya Villafranchian)
  • Gallinula hodgenorum (Hodgen's Waterhen) (New Zealand, mwisho wa Quaternary)
  • Gallinula kansarum (Kansas, MMA, mwisho wa Pliocene)
  • ?Gallinula sp. Viti Levu Gallinule (Fiji , mwisho wa Quaternary; labda Pareudiastes au jenasi mpya)