Fred Ngajiro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Amezaliwa Fred Fabian Ngajiro
Nchi Tanzania
Majina mengine Fred Vunjabei
Kazi yake Mfanyabiashara, Mjasiriamali


Fred Fabian Ngajiro (anajulikana kama Fred Vunjabei; alizaliwa Iringa, Tanzania[1]) ni mfanyabiashara na mjasiriamali kutoka Tanzania[2].

Fred ni Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa kampuni ya Vunjabei (T) Group Limited lakini pia ni mwanzilishi na rais wa kampuni ya Too Much Money Limited. Fred ametajwa kuwa mmoja wa wafanyabiashara wenye umri mdogo na wenye mafanikio makubwa Tanzania.[3]

Maisha binafsi na elimu[hariri | hariri chanzo]

Fred amemaliza digrii ya biashara mwaka 2010 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia shahada ya juu ya usimamizi wa biashara kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2014.[1]

Maisha na biashara[hariri | hariri chanzo]

Punde baada ya kufuzu masomo yake ya chuo mwaka 2014, Fred aliamua kujiajiri kwa kuanza biashara ndogondogo na kwa mtaji mdogo. Alipata nafasi ya kwenda Afrika ya Kusini na simu za rununu aina ya backberry na kuzisafirisha kwenda kuziuza Tanzania na Zanzibar. Biashara haikuwa nzuri sana kwa upande wake ila kwa kile alichokikusanya aliendelea kuwekeza kwenye biashara nyingine ya kuuza magari , kuyachukua kutoka Japan na kuyapeleka Tanzania ili kuyauza. Hapo ndipo biashara ikaanza kukua zaidi na kumuonyesha fursa nyingine. 2015 aliamua kusafiri na kwenda China ili kutafiti juu ya fursa za kibiashara nyingine na ndipo alipogundua kuwa kuna fursa kubwa upande wa mavazi na urembo. Alirudi Tanzania na kuanzisha kampuni yake iitwayo Vunjabei (T) Group Limited na kufungua duka lake la kwanza Kariakoo, Dar es Salaam ambalo lilifanya vizuri na kuweza kuwekeza katika kufungua maduka mengine katika mikoa mbali mbali ya Tanzania.[4]

Licha ya kuwa na maduka mengi ya nguo katika mikoa mbalimbali Tanzania, pia alianzisha kampuni ya usimamizi wa vipaji vya muziki Tanzania inayoitwa Too Much Money Limited ambayo mpaka sasa inamsimamia msanii kutoka Tanzania anayeitwa Whozu.[5]Pia Fred ametajwa kama mmoja wa mabilionea wenye umri mdogo Tanzania kutoka kwenye gazeti la Mwananchi.[6]

Tuzo na Uteuzi[hariri | hariri chanzo]

Fred Fabian Ngajiro amekuwa akiteuliwa katika tuzo mbalimbali za kibiashara na ujasiriamali na baadhi ya tuzo alizochaguliwa kushiriki ni Tanzania Digital Awards ( TDA ) ambayo alishiriki kama Mjasiriamali Bora wa Kiume Kwenye Dijiti (Best Male Entrepreneur on the Digital) mwaka 2019. Pia aliteuliwa kushiriki katika tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards ( TCCA) na alishiriki kama ``Most Preferred Upcoming Male Business Icon Of The Year 2020.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Eafeed Staff (2020-09-29). "Fred Fabian Ngajiro Biography, Age, Education, Career, Family, Net Worth". East African Feed (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2020-10-01. 
  2. 2.0 2.1 "Tanzania's Young Entrepreneur Mr Fred Ngajiro 'Vunjabei' Reveals Secret To His Success - Opera News". ke.opera.news. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2020-10-01. 
  3. Tukohapa. "Fred Fabian Ngajiro: A Famous Tanzanian Businessman who is an Inspiration for Young Entrepreneurs | Tuko Hapa!" (kwa en-GB). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-08-12. Iliwekwa mnamo 2020-10-01. 
  4. "SPLA | Fred Fabian Ngajiro". Spla (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-10-01. 
  5. "Billnass, Young Lunya kumfuata Whozu". Mwanaspoti (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-10-01. 
  6. "Jinsi Fred Vunjabei alivyojenga himaya ya biashara ya Sh4 bilioni". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-14. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]