Nenda kwa yaliyomo

Vunjabei Group Limited

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vunjabei (T) Group Limited pia inajulikana kwa jina la Vunjabei, ni duka la kuuza nguo inayojulikana kwa mavazi ya mtindo wa haraka kwa wanaume, wanawake, vijana na watoto ambayo makao makuu yake yapo jijini Dar Es Salaam, Tanzania. Ilianzishwa na Fred Ngajiro[1], Mtanzania kijana bilionea mwaka 2015. Inajulikana zaidi kwa uuzaji wa nguo kwa bei rahisi nchini Tanzania.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ilianzishwa mwaka 2015 na Fred Ngajiro au kwa jina maarufu Fred Vunjabei ambaye ni mfanyabiashara kutoka Tanzania. Vunjabei ilianzishwa kwa kufungua duka lwa kwanza la nguo ndani ya Kariakoo, Dar es Salaam. Vunjabei ina maduka ya nguo yasiyopungua 15 ndani ya Tanzania na mengine kutajwa kuongezeka Kenya[2]. Licha ya kujulikana kwa kuuza nguo kwa bei rahisi lakini pia Vunjaei inajulikana kwa kutengeneza nguo za michezo kwa klabu za timu ya mpira wa miguu kama Simba Sports Club[3] na Lipuli Football Club.

Ushirikiano

[hariri | hariri chanzo]

Hospitali ya Taifa Muhimbili

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2020, Kampuni ya Vunjabei ilikabidhi zawadi kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila pamoja na watumishi kwa lengo la kuwapongeza na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na watumishi wa afya katika kuwahudumia wagonjwa.[4]

Lipuli Football Club (Lipuli F.C.)

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2020, Vunjabei iliingia makubaliano na timu ya mpira wa miguu LIpuli F.C iliyopo mkoa wa Iringa katika kuwatengenezea nguo za michezo na vifaa vingine vya michezo ikiwemo viatu vya mazoezi, Jezi na kuziuza kupitia maduka ya Vunjabei Nchini kote Tanzania.[5][6]

Simba Sports Club (Simba S.C.)

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2021, Simba Sports Club ilitangaza tenda kubwa kwa makampuni tofauti tofauti katika utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya michezo vitakavyouza na kutumika. Vunjabei iliibuka na kuwa kampuni pekee itakayotengeneza jezi na vifaa vyote vya michezo vya timu ya mpira wa miguuu Simba Sports Club almaarufu kama Simba FC. Vunjabei ilitoa hundi ya pesa za kitanzania Shilingi bilioni mbili [7] . Katika tenda hiyo Vunjabei ilikuwa ikishindana na makampuni zaidi ya 11 kama Umbro na Adidas ambapo Vunjabei iliwezakuchukua nafasi ya juu na kuingia makubaliano na Simba Sports Club (Simba F.C).[8][9][10][11][12]

  1. "Jinsi Fred Vunjabei alivyojenga himaya ya biashara ya Sh4 bilioni". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  2. "Tanzanian fashion icon targets Kenyan market with Vunja Bei stores". Nairobi News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  3. "Vunjabei aimwagia Simba bilioni mbili". www.ippmedia.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  4. "MUHIMBILI BLOG : VUNJA BEI WATOA ZAWADI MLOGANZILA". MNH Official Blog (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  5. "Dar company to support Lipuli FC". www.ippmedia.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  6. "Good News To Tanzania's Lipuli FC As Vunjabei Group Company Chips In For Support - Opera News". ke.opera.news. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  7. "Simba yasaini mkataba wa bilioni mbili na Vunjabei". Simba Sports Club (kwa American English). 2021-04-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-20. Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  8. "Vunjabei aimwagia Simba bilioni mbili". www.ippmedia.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  9. "Simba SC land multi-billion shirt manufacturer deal with Vunjabei | Goal.com". www.goal.com. Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  10. "Tanzanie : Accord de partenariat entre le Simba SC et la société Vunja Bei | Africa Foot United". africafootunited.com (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  11. "Tanzania's Simba SC sign a Multi-billion Deal with Vunjabei Group Limited - Opera News". ke.opera.news. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-21.
  12. "Fred Vunjabei aula Simba, aweka Sh2 bilioni kutengeneza jezi". Mwanaspoti (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-21.


Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vunjabei Group Limited kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.