Frannie Léautier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Frannie Léautier
Amezaliwa
Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro
Nchi Tanzania
Kazi yake Makamu wa Rais Africa Development Bank

Frannie Léautier ni mwanamke wa Tanzania, mhandisi, mtaaluma na mshauri wa maendeleo ya nje, anatumikia kama makamu wa Rais katika Africa Development Bank na ni mmoja kati ya wanabodi wa Bank ya Gavana tangu juni 2016.

Kwa muda wa miaka sita (2001 hadi 2007) aliwahi kufanya kazi kama makamu wa Rais wa taasisi ya Benki ya Dunia. [1][1]

Utoto[hariri | hariri chanzo]

Ni mzaliwa wa Moshi mjini, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa Tanzania. Ana dada wawili na kaka wanne. Akiwa na miaka sita familia yao ilihamia Lushoto iliyopo mlima wa Usambara karibu na hifadhi ya wanyama. Huko alikuwa akiwa na babu yake aliyemshawishi kusoma Fizikia na Uhandisi.[2]

Masomo[hariri | hariri chanzo]

Alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1984 akisomea shahada ya uhandisi wa ujenzi. Aliendelea na masomo katika chuo cha Massachusetts Institute of Technology (MIT), ambapo alisoma shahada yake ya pili ya sayansi ya usafiRishaji mnamo mwaka 1987 na kuhitimu mwaka 1990. [2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Alianza kazi katika Benki ya Dunia mwaka 1994 Washington DC kwa muda wa miaka 15.[3] Baadae aliondoka Banki ya dunia na kuunda kikundi kilichoitwa The Fezembat Group, ambapo alifanya kazi kama msimamizi kwanzia mwaka 2007 hadi 2009. [3][4] Miaka minne baadae kwaanzia Julai 2009 mpaka Novemba 2013, alihamia Harare, Zimbabwe na kufanya kazi kama katibu mtendaji wa the African Capacity Building Foundation, shirika lisilo la faida wakati huo huo alitumikia kama Profesa maarufu wa Sciences Po Paris, kwanzia mwaka 2007 hadi Decemba 2013. Decemba 2013, alirejea nyumbani Tanzania na kutumika kama mwanzilishi mshiriki na mwenyekiti wa Mkoba Private Equity Fund, na alifanya kazi kwa muda wa miaka miwili na nusu mpaka juni 2016. [3]

Ana ufasaha wa lugha za Kiswahili, Kifaransa na Kiingereza, na ana uwezo wa kufanya kazi kwa Kihispania na Kiarabu. [3]

marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 AfDB (22 March 2016). Dr. Frannie Leautier appointed as Senior Vice-President of the African Development Bank Group. African Development Bank Group (AfDB). Iliwekwa mnamo 16 November 2017.
  2. 2.0 2.1 Plaatjes, Elton (1 September 2013). Meet Dr Frannie Léautier – Africa's Queen of Development. Ventures Africa Magazine. Iliwekwa mnamo 16 November 2017.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Léautier, Frannie (16 November 2017). Frannie Leautier: Experienced Executive and Board Member, African Development Bank. Linkedin.com. Iliwekwa mnamo 16 November 2017.
  4. The Fezembat Group (2009). The Fezembat Group: CV Frannie Léautier (Translated from the original French). The Fezembat Group. Iliwekwa mnamo 16 November 2017.