Nenda kwa yaliyomo

Foleti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

 Foleti (Folate), pia inajulikana kama vitamini B9 na folasini,[1] ni mojawapo ya vitamini B.[2] Asidi ya foliki iliyotengenezwa, ambayo hubadilishwa kuwa foleti na mwili, hutumiwa kama kirutubisho cha lishe na katika uimarishaji wa chakula kwani ni thabiti zaidi wakati wa kusindika na kuhifadhi.[3] Foleti inahitajika ili mwili uweze kutengeneza DNA na RNA na kuchakata asidi amino zinazohitajika katika mgawanyiko wa seli.[4] Kwa kuwa wanadamu hawawezi kutengeneza foleti, inahitajika katika lishe, na kuifanya kuwa kirutubisho muhimu.[5] Inatokea kiasili katika vyakula vingi.[1] Kiwango cha ulaji foleti cha kila siku kwa watu wazima nchini Marekani ni mikrogramu 400 kutoka kwa vyakula au virutubisho vya lishe.

Foleti katika muundo wa asidi ya foliki hutumiwa kutibu upungufu wa damu mwilini (anemia) inayosababishwa na upungufu wa foleti.[2] Asidi ya foliki pia hutumiwa kama kirutubisho na wanawake wakati wa ujauzito ili kupunguza hatari ya kutokea kwa kasoro za mirija ya neva (NTDs) kwa mtoto.[2][6] Viwango vyake vya chini katika ujauzito wa mapema vinaaminika kuwa kisababishi cha nusu ya watoto kuzaliwa na kasoro za mirija ya neva (NTDs). Zaidi ya nchi 80 hutumia uimarishaji wa lazima au wa hiari wa vyakula fulani vyenye asidi ya foliki kama hatua ya kupunguza kiwango cha NTDs.[7] Matumizi ya muda mrefu ya kirutubisho cha asidi ya foliki kwa kiasi kikubwa huhusishwa na kupungua kidogo kwa hatari ya kiharusi [8] na kuongezeka kwa hatari ya saratani ya tezi dume.[9] Kuna wasiwasi kwamba kiasi kikubwa cha kirutubisho cha asidi ya foliki kinaweza kuficha upungufu wa vitamini B12.

Kutokula Foleti ya kutosha kunaweza kusababisha upungufu wa foleti. Hii inaweza kusababisha aina fulani ya anemia ambapo seli nyekundu za damu huwa kubwa isivyo kawaida. Dalili zake zinaweza kujumuisha kuhisi uchovu, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kupumua kwa shida, vidonda wazi kwenye ulimi na kubadilika kwa rangi ya ngozi au nywele. Upungufu wa Foleti kwa watoto unaweza kutokea ndani ya mwezi mmoja ya ulaji duni wa chakula.[10] Kwa watu wazima, kiwango cha kawaida cha foleti ya kawaida ya mwili ni kati ya miligramu 10 na 30 (mg), na viwango vya damu vya zaidi ya 7 nmol/L (3 ng/mL).

Foleti iligunduliwa kati ya mwaka wa 1931 na 1943[11] na iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Duniani.[12] Gharama ya jumla ya ununuzi wa virutubisho katika nchi zinazoendelea ilikuwa kati ya dola 0.001 na 0.005 kwa kila dozi kufikia mwaka wa 2014.[13] Neno "folic" linatokana na neno la Kilatini folium (ambalo linamaanisha jani) kwa sababu ilipatikana katika mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi kilichokolea.[14]

  1. 1.0 1.1 "Folate". Micronutrient Information Center, Linus Pauling Institute, Oregon State University. 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 17 Machi 2018. Folate is a water-soluble B-vitamin, which is also known as vitamin B9 or folacin.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Folic Acid". Drugs.com. American Society of Health-System Pharmacists. 1 Januari 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Agosti 2017. Iliwekwa mnamo 1 Septemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Choi JH, Yates Z, Veysey M, Heo YR, Lucock M (Desemba 2014). "Contemporary issues surrounding folic Acid fortification initiatives". Prev Nutr Food Sci. 19 (4): 247–60. doi:10.3746/pnf.2014.19.4.247. PMC 4287316. PMID 25580388.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Bailey LB, Caudill MA (2012). "Folate". Katika Eardman JW Jr, MacDonald IA, Zeisel SH (whr.). Present Knowledge in Nutrition, Tenth Edition. Ames, IA: ILSI Press/Wiley-Blackwell. ku. 321–342. ISBN 978-0-470-95917-6.
  5. Pommerville, Jeffrey C. (2009). Alcamo's Fundamentals of Microbiology: Body Systems. Jones & Bartlett Publishers. uk. 511. ISBN 9780763787127. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.
  6. Bibbins-Domingo K, Grossman DC, Curry SJ, Davidson KW, Epling JW, García FA, na wenz. (Januari 2017). "Folic Acid Supplementation for the Prevention of Neural Tube Defects: US Preventive Services Task Force Recommendation Statement". JAMA. 317 (2): 183–189. doi:10.1001/jama.2016.19438. PMID 28097362.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Wald NJ, Morris JK, Blakemore C (2018). "Public health failure in the prevention of neural tube defects: time to abandon the tolerable upper intake level of folate". Public Health Reviews. 39: 2. doi:10.1186/s40985-018-0079-6. PMC 5809909. PMID 29450103.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  8. Li Y, Huang T, Zheng Y, Muka T, Troup J, Hu FB (Agosti 2016). "Folic Acid Supplementation and the Risk of Cardiovascular Diseases: A Meta-Analysis of Randomized Controlled Trials" (PDF). Journal of the American Heart Association. 5 (8): e003768. doi:10.1161/JAHA.116.003768. PMC 5015297. PMID 27528407. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 27 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2020.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Wien TN, Pike E, Wisløff T, Staff A, Smeland S, Klemp M (Januari 2012). "Cancer risk with folic acid supplements: a systematic review and meta-analysis". BMJ Open. 2 (1): e000653. doi:10.1136/bmjopen-2011-000653. PMC 3278486. PMID 22240654.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Marino BS, Fine KS (2009). Blueprints Pediatrics (kwa Kiingereza). Lippincott Williams & Wilkins. uk. 131. ISBN 9780781782517. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Pond, Wilson G.; Nichols, Buford L.; Brown, Dan L. (2009). Adequate Food for All: Culture, Science, and Technology of Food in the 21st Century (kwa Kiingereza). CRC Press. uk. 148. ISBN 9781420077544. Folic acid's discovery started in 1931...
  12. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
  13. "Folic Acid". International Drug Price Indicator Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 1 Septemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. Chambers Concise Dictionary. Allied Publishers. 2004. uk. 451. ISBN 9788186062364. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)