Florin Andone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andone akiwa Córdoba 2015.

Florin Andone (matamshi ya Kiromania: [floˈrin anˈdone]; amezaliwa 11 Aprili 1993) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Romania ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Uturuki Galatasaray, kwa mkopo kutoka kwa Brighton na Hove Albion. Kimataifa anaiwakilisha timu ya taifa ya Romania.

Florin Andone alilelewa nchini hispania, alianza kucheza katika tarafa za chini za nchi hiyo kabla ya kufanya kazi yake ya kwanza katika timu ya Córdoba akiwa na umri wa miaka 21. Mnamo mwaka 2016, alijiunga na Deportivo La Coruña, na miaka miwili baadaye alisaini kwa Brighton na Hove Albion ya Ligi Kuu.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Florin Andone kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.