Femtomita
Femtomita (ing. femtometer, alama fm[1][2][3]) ni kipimo cha SI cha kutaja urefo mdogo wa 10−15 mita.
Kipimo hiki hutumiwa kwa kutaja vipimo katika fizikia ya atomi na chembe zake.
Kipenyo cha protoni ni takiban femtomita 1.7 [4]. Kipenyo cha kiini cha atomi cha dhahabu ni takriban femtomita 8.45.
Neno latokana na lugha ya (Kidenmark: femten (kumi na tano). Umbali huu unaweza pia kuitwa fermi kwa heshima ya mwanafizikia Enrico Fermi.
Ulinganifu[hariri | hariri chanzo]
femtomita 1 = 1.0 x 10−15 mita = 1 fermi = 0.001 pikomita = 1000 attomita
1,000,000 femtomita = 1 nanomita = 10 Ångström.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-05-23. Iliwekwa mnamo 2014-07-08.
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-07-09. Iliwekwa mnamo 2014-07-08.
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-04-25. Iliwekwa mnamo 2014-07-08.
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-04-23. Iliwekwa mnamo 2014-07-08.