Nenda kwa yaliyomo

Fausta Shakiwa Mosha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fausta Shakwe Mosha)
Faustine Shakiwa Mosha

Amezaliwa
Tanga, Tanzania
Kazi yake Mwandamizi wa juu wa maabara

Fausta Shakiwa Mosha (alizaliwa Mkoa wa Tanga, 14 Aprili 1976) ni Mtanzania anayefanya kazi ya uandamizi wa maabara kwenye shirika la USAPH United State Association of Public Health Laboratories la Afrika Mashariki atika ukanda wa Afrika Kusini. Amekuwa Mkurugenzi wa kituo cha uhakiki na mafunzo ya ubora wa maabara ya Taifa ya Wizara tangu mnamo mwaka 2011.

Historia yake na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Alikulia Moshi huku akipata Elimu yake ya msingi Mkoa Tanga katika shule inayoitwa Tanga International school ambapo hapo baadae alihamia katika shule iitwayo Azimio Primary school kati ya mwaka 1982 mpaka mwaka 1988. Baada ha hapo kati ya mwaka 1989 hadi mwaka 1995 Alijiunga na shule za Kilakala na Loleza hadi apo alipo hitimu elimu yake ya Sekondari.

Alifanikiwa kupata shahada yake ya Udaktari wa dawa yaani doctor of mrdicine (MD) katika chuo kikuu cha Afya cha Muhimbili She obtained her MD from Muhimbili Na alipada Shahada ya uzamivu mwaka 2014 kutoka katika chuo kikuu cha Catholic University of Leuven, Ubeligiji.

Wizara ya Afya

[hariri | hariri chanzo]

Alipewa wadhifa wa ukurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Uhakikisho wa Ubora na Mafunzo ya Afya ya Taifa (NHLQATC) ndani ya Wizara ya Afya MoH, Tanzania mwaka 2010 na mwaka huo huo, alishinda mradi wa kimataifa wa nchi 9 za Kiafrika na nchi 11 katika kanda ya Caribbean.[1]

NHL/QATC

[hariri | hariri chanzo]

Fausta alishawahi fanya kazi katika kusimamia na kuboresha huduma na utoaji wa NHLQATC. Alishiriki kutunga na kuandika makala kadhaa na majarida ya matibabu na kuongoza ushirikiano kati ya CDC na Maabara ya Taifa ya Afya nchini Tanzania.[2]

Miradi mingine

[hariri | hariri chanzo]

Fausta Amekua akisimamia na anaendelea kusimamia miradi ya kitaifa na kimataifa ikiwemo miradi ifuatayo:

Alikuwa Mchunguzi Mkuu (Principal Investigator) wa mradi wa "Uhakiki wa Ufanisi wa Vipimo vya haraka vya VVU, Usalama wa Biolojia wa Baraza la Mawaziri na Baraza la Usimamizi wa Ubora wa Maabara na uimarishaji Tanzania, Uganda, Sierra leone, Cameroon, Angola, Lesotho, Ethiopia, Swaziland, Kenya na Nchi 11 katika ukanda wa Caribbean, mradi ulio na lengo la kuimarisha uwezo wa maabara 9 za Afrika na 11 za Caribbean ili kusaidia kuweka Sura nzuri ya Matibabu[3] Na Alisha wahi kuwa Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Muhimbili cha Tanzania.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fausta Shakiwa Mosha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.