Fausta Shakiwa Mosha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Fausta Shakiwa Mosha (amezaliwa mkoani Tanga nchini Tanzania, 14 Aprili 1976) ni Mtanzania aliye mshauri mwandamizi wa maabara wa chama cha maabara ya afya ya umma ya Afrika mashariki kwa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika. Amewahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Uhakiki wa Maabara ya Afya na Mafunzo ya Wizara ya Afya mwaka 2011 [1].

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Mosha alipata elimu yake katika shule ya kimataifa ya Tanga Tanga International School na baadaye akajiunga na shule ya msingi ya Azimio kati ya mwaka 1982 na 1988 zote Mkoani Tanga.

Kati ya mwaka 1988-1992 alijiunga na shule ya sekondari ya Loleza (Loleza Secondary School) mjini Mbeya na baadaye akajiunga na sekondari ya juu ya Kilakala ndiko alikohitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1995. Alipata shahada yake ya uzamivu udaktari wa afya katika Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili na mnamo mwaka 2014 alipata PhD katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Leuven nchini Ubelgiji.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mboera, LE; Ishengoma, DS; Kilale, AM; Massawe, IS; Rutta, AS; Kagaruki, GB; Kamugisha, E; Baraka, V et al. (2015). "The readiness of the national health laboratory system in supporting care and treatment of HIV/AIDS in Tanzania". BMC Health Serv Res 15: 248. doi:10.1186/s12913-015-0923-z . PMC 4482295 . PMID 26113250 .