Fatuma Abdulkadir Adan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fatuma Abdulkadir Adan (alizaliwa 1978) ni Mkenya mwanasheria na balozi wa amani[1] pia ni mpokeaji wa tuzo ya Stuttgart Peace Prize.[2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Adan alizaliwa na wazazi ambao walikuwa kutoka makabila mawili yanayopigana huko Marsabit, Kenya Kaskazini-Mashariki.

Baada ya masomo yake kama mwanasheria, alirudi katika mji wake ili kukuza amani kati ya wale wanaopigana Waoromo, Wagabra na Warendile.[3] Mnamo 2003, alianzisha Horn of Africa Development Initiative, Shirika Lisilo la Kiserikali aliyotumia kukuza amani na kutetea elimu nchini Kenya.[4]

Kupitia Horn of Africa Development Initiative (HODI), Adan aliuanzisha mpango unaoitwa "Shoot to score, not to Kill", unaotumia soka kuwashirikisha vijana wa Kenya katika utetezi wa amani.[5] Msingi wa Horn of Africa Development Initiative (HODI) una nguzo nne muhimu ambazo ni: Utetezi, Elimu, Uendelevu wa uchumi na Ushirikiano wa kikabila.[6]Kupitia HODI aliianza programu "Breaking the Silence"[7] ambayo ina moduli nne: Kuwa wewe mwenyewe, kuwa na afya, kuwezeshwa na ujue kitu kuhusu fedha. Fatuma Adan ndiye mwanamke wa kwanza wa Kiafrika kuchaguliwa kuwa mwanachama wa Streetfootballworld mnamo 2015.[8]Mwaka wa 2017,aliteuliwa kuwa mmoja wa kundi la kupangia Global Goals World Cup. Mnamo mwaka wa 2011, Adan alipokea tuzo la Stuttgart Peace Prize kwa kujumuisha "soka na ukombozi".[2] 2013, alialikwa kuongelea kazi yake inayohusu Horn of Africa Development Initiative kwenye Mazungumzo ya Amani Mjini Geneva mnamo tarehe 20 Septemba 2013. Mazungumzo yenyewe yalipangwa na Umoja wa Mataifa na vikundi vingine kwa sababu ya Siku ya Kimataifa ya Amani.[9]

Adan alishinda tuzo ya Commonwealth Points of Light Award mnamo 2018 kwa kazi yake ya HODI ya kuzileta jamii pamoja na kupigania haki za wanawake na watoto wa kike.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Stiefel, Sussane. Kenya: Shoot to score, not to kill. Peace Counts. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-07-12. Iliwekwa mnamo 6 February 2016.
  2. 2.0 2.1 Friedenspreisträgerin 2011. Stuttgartr FriedensPreis der AnStifter. Iliwekwa mnamo 6 February 2016.
  3. Williams, Kristin (2 February 2015). Kenyan women among those honoured for promoting peace and inclusivity. African Woman and Child Feature Service. Jalada kutoka ya awali juu ya 6 February 2016. Iliwekwa mnamo 6 February 2016.
  4. Nickerson, Colin (17 February 2015). Four courageous women who are making a difference. Boston Globe. Iliwekwa mnamo 6 February 2016.
  5. Waweru, Kiundu (25 September 2011). Replacing the bullet with football. Standard Media. Iliwekwa mnamo 6 February 2016.
  6. "Fatuma Abdulkadir Adan - Inclusive Security", Inclusive Security. (en-US) 
  7. Fatuma Abdulkadir Adan (en) (2017-07-31). Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-01-26. Iliwekwa mnamo 2021-05-14.
  8. "We Talk With Fatuma Abdulkadir Adan", streetfootballworld. Retrieved on 2021-05-14. (en) Archived from the original on 2018-07-14. 
  9. Fatuma Abdulkadir Adan Archived 10 Julai 2017 at the Wayback Machine., Geneva Peace Talks, UN, Retrieved 27 February 2016
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatuma Abdulkadir Adan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.