Kiajemi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Farsi)
Eneo la Kiajemi

Kiajemi au Farsi (فارسی) ni lugha ya taifa ya Uajemi. Ni kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi, ambazo tena ni kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Inaandikwa kwa herufi za Kiarabu ambamo herufi nne za ziada zimeongezwa kwa kutaja sauti zisizoweza kuonyeshwa kwa Kiarabu asilia. Hizo herufi za ziada ni پ p, چ ch, ژ zh na گ g.

Kiajemi kilikuwa na athira kubwa juu ya lugha mbalimbali hasa Kiarabu na Kituruki.

Inatumiwa hasa katika nchi zifuatazo:

Kuna wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 70, na takriban wasemaji wengine milioni 60 kama lugha ya pili.

  • Katika Afghanistan, yenye wasemaji takriban milioni 15, lugha inaitwa "dari" (درى).
  • Katika Tajikistani, yenye wasemaji milioni 15 pia, lugha inaitwa "Kitajiki".

Kutokana na uhamiaji wa karne ya 20 lugha inapatikana katika nchi nyingi za dunia.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]