Fardosa Ahmed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dokta Fardosa Ahmed alizaliwa mwaka 1985 nchini Kenya ni mjasiriamali, msimamizi wa afya, ambaye anahudumu kama afisa mkuu wa utendaji katika Hospitali ya Premier, Mombasa, kituo binafsi cha afya ambacho yeye ndye muanzilishi na mmiliki.[1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alisomea Shule ya Msingi Makini, jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Kisha alihamia Shule ya Loreto Convent Valley Road, jijini Nairobi, ambako alihitimu stashahada ya Shule ya Upili. Kisha alijiunga katika Chuo Kikuu cha Nairobi, ambako alisomea udaktari wa binadamu, na kuhitimu Shahada ya Udaktari na Upasuaji.[2] Baadaye alipata stashahada ya uzamili katika usimamizi wa afya.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fardosa Ahmed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.