Faraja Kotta
| Faraja Kotta | |
| Amezaliwa | 6 Mei 1985 Dar es Salaam |
|---|---|
| Nchi | Tanzania |
| Kazi yake | Urembo pia ni Mwanachama wa Youth Executive Committee. |
Faraja Kotta (amezaliwa Dar es Salaam, 6 Mei 1985) alikuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2004.
Kotta ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne.
Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi Olympio iliyopo jijini Dar es Salaam, baadae kujiunga na shule ya sekondari St Francis iliyoko mkoani Mbeya kisha kuendelea na elimu ya kidato cha 5 na 6 katika shule ya sekondari ya St Mary's Mazinde Juu, iliyoko Lushoto, Tanga, Tanzania.
Historia ya Urembo
[hariri | hariri chanzo]Kotta aliwahi kuwa "Miss Ubungo" na baadae kuwa "Miss Kinondoni", pia akaja kuchaguliwa kuwa "Miss Tanzania" kwa mwaka wa 2004.
Kazi Tofauti na Urembo
[hariri | hariri chanzo]Kotta ni Mwanachama wa "Youth Executive Committee" ambayo ipo chini ya Youth Net Tanzania, na pia ni Program Officer wa kipindi cha Njia Panda ambapo anafuatilia wale wananchi wanaojitokeza na matatizo na kuhakikisha wamesaidiwa na vipi wanaendelea.
Pia ni mwanzilishi wa programu ya "shule direct" ambayo inasaidia wanafunzi kujifunza masomo yao kupitia mitandao.
Maisha Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 30 Novemba 2007 Faraja alifunga ndoa na mbunge wa Singida, Lazaro Nyalandu.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |