Faraja Kotta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Faraja Kotta (amezaliwa Dar es Salaam, 6 Mei 1985) alikuwa mrembo wa Tanzania mwaka 2004.

Kotta ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne.

Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi Olympio iliyopo jijini Dar es Salaam, baadae kujiunga na shule ya sekondari St Francis iliyoko mkoani Mbeya kisha kuendelea na elimu ya kidato cha 5 na 6 katika shule ya sekondari ya St Mary's Mazinde Juu, iliyoko Lushoto, Tanga, Tanzania.

Historia ya Urembo[hariri | hariri chanzo]

Kotta aliwahi kuwa "Miss Ubungo" na baadae kuwa "Miss Kinondoni", baada ya kuwa Miss Kinondoni akaja kuchaguliwa kuwa "Miss Tanzania" kwa mwaka wa 2004.

Kazi Tofauti na Urembo[hariri | hariri chanzo]

Kotta ni Mwanachama wa "Youth Executive Committee" ambayo ipo chini ya Youth Net Tanzania, na pia ni Program Officer wa kipindi cha Njia Panda ambapo anafuatilia wale wananchi wanaojitokeza na matatizo na kuhakikisha wamesaidiwa na vipi wanaendelea.

Maisha Binafsi[hariri | hariri chanzo]

Faraja tarehe 30 novemba 2007 alifunga ndoa na mbunge wa Singida, Lazaro Nyalandu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]