Nenda kwa yaliyomo

Familia ya Karimjee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Familia ya Karimjee ni familia ya wafanyabiashara inayomiliki kampuni ya Karimjee Jivanjee Limited [1] inayojihusisha na biashara mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo usafirishaji, masoko ya fedha na uwekezaji.[2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ya Karimjee Jivanjee Limited ilianzishwa na Karimjee Jivanjee mwaka 1861. Kabla ya hapo, baba yake, Budhaboy Jivanjee, aliyehamia Zanzibar kutoka Mandvi, Gujarat, mwaka 1818, alianzisha biashara ya Budhaboy Jivanjee & Co mwaka 1825. Kupitia biashara hiyo alikuwa akiuza nguta na karafuu kwenda India na kuingiza na kuuza bidhaa za nguo kutoka Marekani na Ujerumani.

Kampuni ya Karimjee & Co. iliyoanzishwa mwaka 1861 Zanzibar iliendelea na biashara ya usafirishaji wa bidhaa kwenda na kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Shelisheli, Morisi na Ceylon. Kampuni ya Karimjee walikuwa wakitumia mashua aina ya jahazi kusafirisha bidhaa Pwani ya Waswahili [2]

  1. "Growing Together | Karimjee Jivanjee". web.archive.org. 2024-02-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-27. Iliwekwa mnamo 2024-09-10.
  2. 2.0 2.1 Oonk, Gijsbert (2009). The Karimjee Jivanjee Family, Merchant Princes of East Africa. Amsterdam: Amsterdam University Press. {{cite book}}: Check |author-link= value (help); External link in |author-link= (help)