Nenda kwa yaliyomo

Evangeline Lilly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Evangeline Lilly

Amezaliwa 3 Agosti 1979
Fort Saskatchewan, Alberta, Canada
Kazi yake Mwigizaji

Nicole Evangeline Lilly (amezaliwa Agost 3, 1979) ni mwigizaji wa kutoka Canada aliyepata umaarufu kutokana na kuigiza kwake kama Kate Austen kwenye kipindi cha Lost.

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Lilly alizaliwa mjini Fort Saskatchewan katika nchi ya Canada kutokana na familia ya Kikristo. Babake ni mwalimu, na mamake ni mtu wa mwanamitindo. Lilly ana dada wawili. Katika maisha yake ya utotoni, familia yao haikuwa na runinga.[1]

Uigizaji

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni, Lilly alikuwa mwanamitindo. Alijiunga na Ford Models kama mwanamitindo, lakini akabadilisha mwenendo na kuwa mwigizaji wao.[2]

Mshahara wake wa Lost ni $80,000 kila kipindi. Kwa ajili ya Lost, alichaguliwa kama Breakout Stars of 2004 na Entertainment Weekly.Lilly amewekwa namba 13 kwenye orodha ya FHM "100 Sexiest Women in the World" mnamo 2006 na hapo awali alikuwa namba 2 kwenye orodha ya Maxim's "Hot 100" mnamo 2005.[3]

Maisha yake ya kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]

Lilly alikuwa ameolewa na Murray Home, lakini wameachana.[4] Tangu 2004, amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji-mwenza wa Lost aitwaye Dominic Monaghan.

Mnamo 20 Desemba 2006, nyumba yake mjini Hawaii ilichomeka alipokuwa akirekodi Lost..[5] Chanzo cha moto huu ilisemekana kuwa ni hitilafu ya stima.

  • Alichaguliwa kwa 2007 Golden Globe Award: Best Actress in a Drama lakini hakushinda.
  • Alishinda tuzo la 2007 Screen Actors Guild Award: Outstanding Performance by Ensemble Cast in a Drama Series.
  • Alichaguliwa kwa tuzo la 2005 Satellite Award: Best Actress in a Drama lakini hakushinda.
  • Alichaguliwa kwa tuzo la 2006 National Television Award:Most Popular Actress lakini hakushinda.
  • Hivi sasa, amechaguliwa kwa tuzo la 2010 Screen Actors Guild Award: Outstanding Performance by a Cast in a Motion Picture.
Lilly kwenye tuzo ya Emmy Awards
Filamu
Mwaka Filamu Aliigiza kama Maelezo
2003 The Lizzie McGuire Movie Afisa wa polisi
Stealing Sinatra Mwanamitindo
Freddy vs. Jason mwanafunzi Standing next to locker (Uncredited)
2005 The Long Weekend Simone
2008 Afterwards Claire
The Hurt Locker Connie James
2011 Real Steel
Filamu
Mwaka Filamu Anaigiza kama Vipindi
2002 Reviews on the Run JD Girl 1
Smallville kwenye vipindi vya "Visage" na "Kinetic" 3
2003 Tru Calling mgeni 1
2004 Kingdom Hospital mpenzi wa Benson 1
2004 - 2010 Lost Kate Austen 114
2007 Punk'd mwenyewe 1
  1. "INS News". I'M NOT JUST Lost PROPERTY; She May Be One of the Hottest Young Actresses in Hollywood, but Lost St... Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-14. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2006. {{cite web}}: Unknown parameter |dateformat= ignored (help)
  2. Brady, James. Evangeline Lilly (Canadian TV and film actress), Parade, 23 Oktoba 2005. Accessed 26 Mei 2008.
  3. Evangeline Lilly makes Maxim Hot 100, CBC Arts | this link does not work anymore
  4. Gould, Lara. Exclusive: I Got So Famous I Nearly Lost It, Sunday Mirror, 19 Novemba 2006. Accessed 26 Mei 2008.
  5. Dondoneau, Dave; Ritz, Mary Kaye. Fire destroys home of 'Lost' actress Lilly, The Honolulu Advertiser, 20 Desemba 2006. Accessed 26 Mei 2008.