Ana Lucia Cortez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ana Lucia Cortez
Mwonekano wa kwanza"Exodus: Part 1"
Centric
episode(s)
"Collision"
"Two for the Road"
Maelezo
JinaAna Lucia Cortez
Umri29
Zamani
makazi
Los Angeles, California, USA
(Taaluma) ya zamaniAfisa wa polisi kwenye LAPD
Airport security guard
Imechezwa naMichelle Rodriguez

Ana Lucia Cortez ni jina la mhusika wa kipindi maarufu cha televisheni cha Kimarekani cha Lost ambacho hurushwa hewani na ABC. Uhusika umechezwa na Michelle Rodriguez. Ana Lucia alianza kuonekana katika kipindi cha mwisho wa msimu wa kwanza wa mfululizo huu. Baada ya ajali, ndege ya Oceanic 815 ilipasuka mara mbili: kichwa na mkia wa ndege hii ilianguka mahali pawili tofauti. Ana Lucia ndiye aliyekuwa akiwaongoza waathiriwa waliotokamana na mkia wa ndege hii. Kabla ya ajali hii, Ana Lucia alikuwa akifanya kazi kama afisa wa polisi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ajali ya Oceanic 815, Ana Lucia alikuwa afisa wa LAPD. Alikuwa na mimba, lakini mimba hii ilitoka baada ya kupigwa risasi na majambazi. Hatimaye, Ana Lucia aliwacha kazi LAPD na kujiunga kama afisa wa uwanja wa ndege. Alikutana na Christian Shepherd anayemuomba awe mlinzi wake pindi atakapoenda Sydney.

Baada ya ndege ya Oceanic kuanguka baharini, Ana Lucia anajaribu kadri awezavyo kuwaokoa wenzake.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Michelle ROdriguez alishinda tuzo la "ALMA Award" ya "Outstanding Supporting Actress in a TV Series".[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "2006 Award Winners", National Council of La Raza. Retrieved on 2008-03-04. Archived from the original on 2008-02-29.