Esopi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kigezo:Tfm

Esopi, Aesop
Αἴσωπος (Aisōpos)
Sanamu ya Esopi, mnamo karne ya 1 BK, Villa Albani, Roma
Bornc. 620 KK
Died564 KK (umri wa miaka 56)
Delphi, Greece
NationalityUgiriki
GenresFable

Esopi, pia Aesop (kutoka kwa Kigiriki Αἴσωπος, Aisopos), alikuwa mshairi wa Ugiriki wa Kale. Ni maarufu kwa ngano zake. Anasemekana alikuwa mtumwa mwenye asili ya Thrakia ambaye aliishi kutoka karibu 620 KK hadi 560 KK katika Ugiriki ya Kale .

Ngano za Esopi huwa na mafundisho mengi ya kimaadili. Wahusika katika masimulizi yake mara nyingi ni wanyama au vitu vinavyoweza kuongea, kupata usuluhisho wa matatizo mbalimbali na hivyo kuonyesha tabia za kibinadamu.

Kuna ngao na hadithi elfu zilizosemekama alizitunga, ingawa hakuna uhakika kama mwenyewe aliandika kitu chochote au kama alikusanya tu masimulizi yaliyokuwepo tayari.

Hadithi zake maarufu zaidi ziko pamoja na "Simba na Panya" au "Kobe na Sungura". Sungura anataka kushindana na kobe kwa mbio akiwa na uhakika atashinda. Kwa hiyo hajitahidi, anatumia nafasi ya kulala usingizi njiani hadi anaona mwishowe kwamba kobe ni mshindi kwa sababu sungura alijiamini mno.

Ngano za Aesop[hariri | hariri chanzo]

Aesopus moralisatus, 1485

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Caxton, John, 1484. Historia na hadithi za Aesop, Westminster. Uchapishaji wa kisasa uliohaririwa na Robert T. Lenaghan (Chuo Kikuu cha Harvard Press: Cambridge, 1967).
  • Bentley, Richard, 1697. Utaftaji juu ya Nyaraka za Phalaris ... na Hadithi za Æsop . London.
  • Jacobs, Joseph, 1889. Hadithi za Aesop: Zilizochaguliwa, Kuambiwa Upya, na Historia Yao Zilizofuatiliwa, iliyochapishwa kwanza na William Caxton, 1484, kutoka kwa tafsiri yake ya Kifaransa
  • Handford, SA, 1954. Ngano za Aesop . New York: Ngwini.
  • Perry, Ben E. (mhariri), 1965. Babrius na Phaedrus, (Loeb Classical Library) Cambridge: Harvard University Press, 1965. Tafsiri za Kiingereza za hadithi 143 za hadithi za Kigiriki na Babrius, hadithi 126 za Kilatini na Phaedrus, hadithi 328 za Uigiriki ambazo hazipo Babrius, na hadithi 128 za Kilatini ambazo hazipo katika Phaedrus (pamoja na vifaa vya medieval) kwa jumla ya hadithi 725.
  • Hekalu, Olivia na Robert (watafsiri), 1998. Aesop, Hadithi Kamili, New York: Classics za Penguin. (  )

Tovuti nyingine[hariri | hariri chanzo]