Nenda kwa yaliyomo

Maporomoko ya Kalambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maporomoko ya Kalambo.

Maporomoko ya Kalambo yanatokana na mto Kalambo ambao ni mpaka wa Tanzania na Zambia.

Maporomoko ya maji hayo ya mita 235 kwa mkupuo mmoja, ukiachilia kuwa ni ya pili baada ya yale ya Tugela (Afrika ya Kusini), lakini pia ndiyo maporomoko pekee yanayogawa nchi mbili.

Maporomoko hayo yapo katika kijiji cha Kapozwa, kata ya Kisumba, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa. Katika kijiji cha Kapozwa, ambacho kilianzishwa kutokana na imani kuwa ukienda kuoga katika maporomoko hayo utapooza. Kwa kuambiwa hivyo wenyeji wa eneo hilo walipaita kijiji jina la Kapozwa.

Maporomoko hayo yamekuwa yakionekana na kutangazwa kuwa yapo Zambia na hivyo kuiondoa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye maporomoko yanayotambulika duniani.

Eneo la akiolojia[hariri | hariri chanzo]

Maporomoko ya Kalambo ni pia eneo la kiakiolojia katika kata ya Kapele, Wilaya ya Kalambo, ndani ya Mkoa wa Rukwa, Tanzania.

Profesa John Desmond Clark alichunguza eneo hilo kuanzia mwaka 1956 hadi 1959. Uchimbaji katika viunga vya ziwa ulifichua mlolongo wa enzi ya mawe kutoka enzi ya kale ya mawe hadi enzi ya chuma, na nyingi zikiwa zimetapakaa katika sakafu za makazi katika eneo hlo.[1][2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kalambo Prehistoric site". unesco.org. Iliwekwa mnamo 2022-06-01.
  2. Gabel, Creighton. The International Journal of African Historical Studies, vol. 35, no. 2/3, 2002, pp. 543–46. JSTOR, https://doi.org/10.2307/3097663. Accessed 11 Jun. 2022.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maporomoko ya Kalambo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.