Eneo la Biashara Huria Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rangi ya kijani inaonyesha Eneo la Biashara Huria Afrika.

Eneo la Biashara Huria Afrika (pia: Eneo la Biashara Huria la Kiafrika; kifupi: AFTZ ) ni eneo la biashara huria lililotangazwa katika Mkutano wa (EAC-SADC-COMESA) tarehe 22 Oktoba mwaka 2008 na wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na Kusini (COMESA) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mnamo Mei mwaka 2012 wazo hilo lilijumuisha pia ECOWAS, ECCAS na AMU.[1]

Mnamo Juni mwaka 2015, katika Mkutano wa Umoja wa Afrika nchini Afrika Kusini, waliziundua Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (cfta) ya nchi zote 55 za Umoja wa Afrika ifikapo mwaka 2017.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Africa free trade zone in operation by 2018. Xinhua News Agency (26 May 2012). Iliwekwa mnamo 2012-06-21.
  2. "Launch of the Continental Free Trade Area: New prospects for African trade?", International Centre for Trade and Sustainable Development, 23 June 2015. Retrieved on 26 December 2015.