Elsie Kanza
| Elsie Kanza | |
| Amezaliwa | nchini Kenya |
|---|---|
| Nchi | Tanzania |
| Kazi yake | balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Marekani kutoka mwaka 2021 |
Elsie Kanza ni mwanauchumi Mtanzania aliyezaliwa Kenya. Elsie ni Mkurugenzi mkuu wa Jukwaa la Uchumi wa Nchi za Afrika (World Economic Forum[1]) tangu mwaka 2014.
Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes alitajwa kama mmoja kati ya Wanawake 20 Vijana wenye Nguvu Afrika kwa mwaka 2011.[2]
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Kanza alizaliwa nchini Kenya na wazazi wenye asili ya Tanzania, akapata elimu yake nchini Kenya na baadaye kuendelea na masomo nchini Marekani.
Kwa kipindi cha miaka 1997-2006, Elsie aliweza kupata shahada ya biashara na utawala wa kimataifa katika chuo kikuu cha United States International – Afrika, shahada ya uzamili ya sayansi ya fedha katika chuo cha Strathclyde na shahada ya uzamili katika sanaa ya maendeleo ya kiuchumi katika chuo cha Williams cha nchini Marekani.[3]
Ameweza kupata nafasi mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na kuwa mshauri wa masuala ya uchumi wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa miaka 2006-2011. Pia Ni balozi mteule wa Tanzania nchini Marekani. Ameteuliwa tarehe 17/08/2021 na kuapishwa tarehe 21/08/2021[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.lionessesofafrica.com/blog/2016/5/18/quote-of-the-day-by-elsie-kanza
- ↑ https://www.forbes.com/sites/faraigundan/2013/06/17/meet-elsie-kanza-head-of-africa-at-the-world-economic-forum-on-delivering-on-africas-promise/#1268ca9e7fcc
- ↑ https://www.huffingtonpost.com/ebenezar-wikina/wef-africa-at-25-my-strol_b_8508140.html
- ↑ https://www.weforum.org/agenda/authors/elsiekanza/
| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |