Nenda kwa yaliyomo

Elamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Elam)
Ramani inayoonyesha eneo la Milki ya Elamu (katika nyekundu) na maeneo ya jirani.

Elamu ilikuwa ustaarabu wa kale mashariki mwa Mesopotamia. Elam ilienea katika magharibi na kusini-magharibi mwa Iran ya sasa, pamoja na sehemu ndogo ya kusini mwa Iraki. [1]

Mji muhimu zaidi ulikuwa Shushani; kwa karne kadhaa mji mkuu ulikuwa Dur-Untash kilomita 40 kusini mwa Shushani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Elamu inajulikana kwa sehemu tu. Ilidumu zaidi ya milenia 2. Wataalamu hugawa historia hiyo kwa vipindi vifuatavyo:

  • Proto-Elamu: mnamo 3200 KK - 2700 KK (mjini Shushani maandishi na michoro vinapatikana ambavyo ni tofauti na Uruk)
  • Elamu ya Kale: 2700 KK - 1600 KK (nchi ilivamiwa mara kadhaa na watawala kutoka Mesopotamia, mara chache ilijitawala na hata kudhibiti sehemu za Mesopotamia)
  • Elamu ya Kati: 1500 KK - 1100 KK (watawala wa Elamu hupanua utawala juu ya sehemu kubwa zaidi za Mesopotamia; hatimaye mtawala wa Babeli alivamia Shushani)
  • Kipindi cha Neo-Elamu: 1100 KK - 539 KK (mapambano dhidi ya milki mpya ya Ashuru, hatimaye kuvamiwa na kuharibika na Ashuru)

Rekodi zilizoandikwa huanza kutoka karibu 3000 KK katika kipindi cha Waelami wa Kale (Zama za Shaba ya Kati). Katika Milki ya Waakhameni lugha ya Kielamu ilikuwa miongoni mwa lugha zilizotumika rasmi. Lugha ya Kielamu haina uhusiano unaoeleweka na nyingine yoyote.

Waelamu waliita nchi yao "Haltamti", lakini Wasumeri na Waakadia waliiita Elamu, na ndivyo ilivyoitwa pia katika Biblia ya Kiebrania.

Ustaarabu wa Elamu ulianza karibu 2700 BC, na hatimaye walishindwa na Waakhameni mnamo 640 KK. Kibao kilichopatikana mwaka wa 1848 kina mfalme wa Ashuru Ashurbanipal akijigamba juu ya ushindi wake:

  1. Potts D.T. 1999. The Archaeology of Elam: formation and transformation of an ancient Iranian state. Cambridge World Archaeology.