Eddi Reader
Sadenia "Eddi" Reader (alizaliwa 29 Agosti 1959)[1] ni mwimbaji-mtunzi wa nyimbo wa Uskoti, anayejulikana kwa kazi yake kama mwanamke mwenye mchango mkubwa katika Fairground Attraction na kwa kazi ya kudumu ya kipekee. Yeye ndiye mpokeaji wa tuzo tatu za BRIT. Mnamo 2003, alionyesha kazi za mshairi wa kitaifa wa Uskoti, Robert Burns.
Awali
[hariri | hariri chanzo]Reader alizaliwa Glasgow, uskoti, ni mtoto wa kike wa welder, na mtoto mkubwa wa watoto saba kwao[2] (kaka yake, Francis Reader, ni mtu wa vocal kwenye bendi ya muziki ya "The Trash Can Sinatras" na bibi yake, Sadie Smith, alikuwa ni kiongozi katika timu ya mpira ya Uskoti.[3]). Alipewa jina la utani la Edna na wazazi wake. Aliishi katika wilaya ya Anderston 1965, na baadae familia yao ilihamia kwenye nyumba ya vitanda viwili huko Arden, Glasgow.[4]
Kufikia mwaka 1976,familia yao ilihamia Irvine maili 25 kutokea Glasgow kutokana na idadi kubwa ya watu na msongamano. Japokuwa Reader alirejea Glasgow (ambapo aliishi na bibi yake huko Pollok) akimalizia masomo yake ya shule ya msingi.[4][5] Alianza kujifunza na kucheza gitaa alivyokuwa na umri wa miaka 10,na kuanza safari yake ya muziki, akicheza na kupiga muziki mitaani na barabarani, mwanzo ilikuwa ni huko Glasgow katika mtaa wa Sauchiehall na baadae katika miaka ya mwanzoni ya 1980 akiwa mjini London,Uingereza na Ulaya, akifanya kazi pia katika vikundi vya sanaa.
Huko Scotland, alipokuwa akitafuta kazi ya kiwandani huko Irvine na kufanya kazi kwa muda katika Studio ya Kurekodi ya Sirocco huko Kilmarnock, alijibu tangazo kwenye vyombo vya habari vya muziki, na akasafiri hadi London kufanyiwa majaribio na kujiunga na bendi ya "post-punk Gang of Four", ambao walihitaji mwimbaji kwaajili ya kipindi cha muziki cha televisheni cha Uingereza The Old Gray Whistle Test na pia kwaajili ya ziara yao ya Uingereza. Hii ilisababisha ziara yake ya kwanza ya Marekani na bendi hio. Baada ya kurudi Uingereza na kuacha bendi, alianza kufanya kazi kama mwimbaji wa baadhi ya vipindi huko mjini London, akichukua kazi ya kuimba nyimbo za matangazo ya redio na kuimba nyimbo kama vile "Eurythmics", "The Waterboys", "Billy MacKenzie", "John Foxx" na "Alison Moyet".[6]
Fairground Attraction
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1984, Reader alirudi Uingereza kutokea Paris, ambapo alikuwa akifanya kazi kama mwimbaji wa mtunzi Vladimir Cosma. Kupitia mawasiliano yake na wachezaji wa muziki maarufu kama "The Kick Horns" wa huko London, alitia saini mkataba na EMI, na kurekodi nyimbo mbili na kundi la "Disco Outbar Squeek". Wakati huohuo, alikutana na kumwomba Mark E. Nevin, mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo kutoka bendi ya Jane Aire na Belvederes kumwandikia na wakarekodi nyimbo mbili kama 'The Academy of Fine Popular Music'. Baadaye waliunda Fairground Attraction, pamoja na Simon Edwards (gitarrón - gitaa la besi ya akustisk ya nchini Meksiko) na Roy Dodds (ngoma na midundo). Mnamo 1988 bendi ilitia saini na kuitwa RCA/Bertelsmann Music Group na kurekodi na kutoa wimbo wao wa kwanza, "Perfect", ambao ukawa nambari moja wa Uingereza,[7]kushinda wimbo bora zaidi wa 1989 kwenye tuzo za BRIT. Albamu yao ya kwanza, The First of a Million Kisses, pia ilifanikiwa, na kufikia nambari mbili katika chati ya albamu za Uingereza, na kushinda albamu bora zaidi katika tuzo za Brits za 1989.
Mafanikio haya yalikuwa ya muda mfupi, hata hivyo. Mnamo Novemba 1989, baada ya mapumziko, wakati Reader alipata mtoto wake wa kwanza, Charlie, na mwenzi wake mwenye asili ya kifaransa na Algeria Milou, mabishano yalizuka ndani ya kikundi, na Nevin akaachana na kipindi cha kurekodi albamu ya pili, ambayo hatimaye ilisababisha kugawanyika bendi hio.[7] Albamu ya pili yenye, mkusanyiko wa nyimbi za "B-sides" na nyimbo za jukwaani, Ay Fond Kiss, ilitolewa haraka mwaka uliofuata.
Kazi za peke yake
[hariri | hariri chanzo]Mirmama na Eddi Reader (1992–1994)
[hariri | hariri chanzo]Reader alirudi Uskoti, lakini kabla ya kuanza kazi yake ya peke yake alichukua mkondo wa muda katika kuigiza. Aliigiza Jolene Jowett, mwimbaji na mcheza kinanda cha mkono, katika igizo la Your Cheatin' Heart la John Byrne, mfululizo wa tamthilia ya uchekeshaji ya kwenye Televisheni ya BBC, iliyowekwa katika eneo la muziki nchini uskoti. Mnamo 1993 Reader alikuwa mtangazaji wa BBC ya Uskoti katika kipindi cha "No Stilettos". ,[8] programu ya muziki iliyorekodiwa huko Glasgow. Sifa zake nyingine za uigizaji ni pamoja na kucheza ama kuigiza sehemu ya Joy 3 kutoka kwa Michael Boyd (mkurugenzi wa kisanii wa "Royal Shakespeare Company") utayarishaji wa The Trick Is to Keep Breathing ya Janice Galloway.[7] Hili lilikuwa toleo la BBC Radio 4 mwaka wa 1996 na pia utayarishaji wa "Tron Theatre" mwaka huo huo.
Baada ya kurudi London, Reader alifanyia kazi nyenzo mpya ya muziki na bendi inayojiita "The Patron Saints of Imperfection" (iliyoundwa na Roy Dodds, Neill na Calum MacColl, na Phil Steriopoulos).[7] Hii ikawa albamu yake ya kwanza ya peke yake, iliyorekodiwa na lebo ya muziki ya RCA: Mirmama ya 1992.[7] Alikutana na Geoff Travis ambaye alimtia saini kwenye lebo ya "Warner Brothers" na katika lebo ndogo, "Blanco Y Negro".[7] Mkurugenzi mkuu Rob Dickens alitayarisha albamu yake ya pili ya peke yake Eddi Reader (1994), ambayo ilimshindia muimbaji bora wa kike katika tuzo za BRIT kwa mwaka huo, ikifuatiwa na Candyfloss and Medicine (1996), na Angels & Electricity (1998).[7] Aliachana na "Warner Brothers" na kuendelea na kazi yake ya mwenyewe kwenye lebo ya Geoff Travis ya "Rough Trade" aliporekodi Simple Soul (2001) na Driftwood (2002) - toleo la "nyumbani" la nyimbo zilizorekodiwa wakati wa vipindi vya Simple Soul. Wakati huu, Reader pia alirekodi wimbo "Ocean Love" kwa ajili ya kutumika kwenye filamu ya Help! I'm a Fish (2001).[onesha uthibitisho] Reader pia alichangia sauti yake katika mojawapo ya nyimbo za mwisho za "Big Country" kabla ya kifo cha Stuart Adamson.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Eddi Reader biography, up to 2000". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Novemba 2009. Iliwekwa mnamo 28 Agosti 2009.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help) - ↑ O'Rourke, Lynn. "Q & A with Eddi Reader", The Scotsman, 1 April 2007.
- ↑ "Football was 'quite unsuitable' for women… or so they said". STV News (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2021-12-03. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ 4.0 4.1 My Schooldays: Eddie Reader, The Scotsman, 22 May 2002
- ↑ "Sings the songs of Robert Burns", 12 May 2003. Retrieved on 2023-04-04. Archived from the original on 2008-11-19.
- ↑ "Eddi Reader at NME". NME. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Novemba 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 7.6 Colin Larkin, mhr. (1997). The Virgin Encyclopedia of Popular Music (tol. la Concise). Virgin Books. uk. 999. ISBN 1-85227-745-9.
- ↑ "Rock makes a point with No Stilettos". HeraldScotland. Iliwekwa mnamo 21 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eddi Reader kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |