Dom Down Click

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dom Down Click
Logo ya DDC.
Taarifa za awali
ChimbukoDodoma, Tanzania
Miaka ya kazi2013-hadi sasa
StudioAJ Records, M Lab
Ameshirikiana naOne Incredible, Songa, Kadi-Go, Bin Simba, Mr. II, Da Vinci

Dom Down Click (hufupishwa: DDC) ni jina la kikundi cha harakati za muziki wa hip hop kutoka Dodoma, nchini Tanzania.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya wanachama wa DDC.

Jina la DDC limebuniwa na Lucas Malali, maarufu kama LC. Kundi linatokana na makutano ya kila siku maskani kwao huko Dodoma, hatimaye likaja wazo la kuanzisha harakati za kughani (kurap). Ili kuunda kundi, ilikuwa ni lazima akutane na marafiki ili kukamilisha harakati hizi mwanana. Baada ya kughani wakiwa maskani kwa muda mrefu, ndipo lilipokuja wazo la kwenda kurekodi. Bahati nzuri, LC alikuwa na rafiki yake mmoja mtayarishaji wa rekodi maarufu kama Abuu. Suala la Abuu kufungua studio (AJ Records), imekuwa heri kwa LC na wana DDC kwa ujumla. Huko maskani, kulikuwa na marafiki wengi tu waliokuwa wanaghani, lakini LC alikuwa hajui kama wanaghani.

Baada ya makutano ya mara kadhaa, likaja suala la kwenda kurekodi ndipo sasa baadhi ya marafiki wa pale kitaa wakajitokeza kama na kujulikana kama nao waghanaji. Watu hao waliojitokeza baada ya azimio la kwenda studio ni pamoja na Adam Shule Kongwe, Dilema Bonito, Goda, Badi, K2da, na Andre K. wote wakiwa chachu kubwa kuazisha hizi harakati kwa pamoja wakakubaliana waende kurekodi na wakafanikiwa kurekodi wimbo wa kwanza uliyokwenda kwa jina la "Usika wa Manane". Kwa bahati mbaya, wimbo huo haujafanikiwa kutolewa. Baada ya kufanikisha ngoma ya kwanza, uraibu wa kurekodi wimbo mwingine zaidi ukawajia. Ikawa kawaida sasa kila Jumapili kwenda studio na kuanza kurekodi ngoma mbalimbali kwa kutumia biti za mbele. Baada ya kurekodi nyimbo kibao, wakaona sasa inafaa sasa kuachia ngoma kutoka katika kundi, ndipo walipotoa "Fikra za Wazawa" ambayo ndani yake kulikuwa na Badi, Kagusa, Koku, SlimSal. Ili kuandaa ngoma hii ilibidi watumie biti la Duke ambalo walilitumia bila idhini yake. Biti hilo walilichukua katika mafaili ya Nash MC wakati huo alivyoenda Dodoma. Biti hilo hajachukua idhini ya Nash wala Duke.

Ilitokea tu ameikwara kutoka katika mafaili ya Nash. Isitoshe Nash tayari alikuwa keshamwachia mazagazaga kibao. Mdundo huo jumlisha balaa walilolifanya kwenye biti, wakaona heri waachie tu kwenye maredio. Waliendelea zaidi kuitoa kwenye mitandao hadi wakati ambao akina Tamaduni Muzik walivyoenda kufanya tamasha lao huko Dom, wakaganda pia ili wafanye nao japo ngoma moja, wakafanya "Colabo Mdundo" ambayo ilifanywa na Andre K na Adam Shule Kongwe. Wimbo huo ndio ngoma yao ya pili. Baada ya harakati kuwa kubwa na kufahamika kwao kukawa kumeongezeka lakini shida ikawa kwenye jina la kundi.

Asili ya jina[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kutoa nyimbo kaadhaa, nyimbo zilikuwa zinapigwa lakini waliochana kina nani ilikuwa kigugumizi kidogo. Kuanzia hapo, ndipo walipoanza sasa mchakato wa kutafuta jina ambalo litafaa kwa ajili ya kundi. Hata kuanzisha kundi rasmi lilikuja baada ya kutafuta jina la kundi. Baada ya majadiliano wakaona bora waje na jina la Dom Down Click, ambalo hasa limelenga harakati za hip hop zinazofanyika jijini Dodoma. Kiufupi, Dom ina maanisha Dodoma, Down walimaanisha kama wasanii wachanga wanaolianzisha minukisho jijini humo na Click ilitumiwa kama sehemu ya familia moja. Kuanzia hapa sasa, hamasa ikawa kubwa na kila mtu aliyependa kujiunga na harakati alikaribishwa. Baadaye wakaja akina Saliloo, Therapist, Miracle. Halafu wakaja akina Bin Laden, kabla kuendeleza harakati zake upande mwingine na kutoka Click rasmi.

Watayarishaji wa DDC na albamu za awali[hariri | hariri chanzo]

Watayarishaji wa DDC ni watu mbalimbali, lakini karibia asilimia 80 ya nyimbo za DDC zimefanywa na Bin Laden na AJ, lakini baadaye harakati zilienea na kufanikiwa kupata nafasi ya kukutana na Duke katika studio ya AJ. Duke alihitaji kujua nia ya dhati ya wana katika suala zima la kufanya hip hop. Majibu yao, yalimfurahisha Duke (upenzi utamaduni wa hip hop), na hapa ndipo alipowapa ofa ya kuandaa kandamseto mmoja ambayo ndio "The Element Volume II". Wakati The Element Volume I ambayo Duke aliiandaa kwa ajili ya Tamaduni Muzik hasa One Incredible, Nikki MbishI, Stereo na kushirikisha wasanii wengine kama vile Grace Matata, Izzo Business, Chidi Benz, Suma, Domo Kaya na Goapele. Wakiwa na Duke walifanikiwa kutengeneza nyimbo takriban 13, safari hii haijaenda bure. Hii ilifanya vizuri sana na watu wengi sasa waliwajua DDC. Baada ya mzigo kukamilika wakafanya uzinduzi (albamu walifanya 2014). Wakaingiza mzigo sokoni, halafu baadaye wakarudi tena wao kama wao. Sehemu kubwa ya albamu hii walifanya na Belo na Bin Laden. Albamu ilikwenda kwa jina la "Mechanism" yenye nyimbo 21. Ngoma zilizoachiwa kama single kutoka katika albamu ni pamoja na "Kata Nyau", "Mitambo", "Masudi", "Punch Norris", Noma na nyengine kibao. Wakati huu DDC inazidi kuyoyoma angani, wakaja wakatoa "Fasihi Simulizi" ambayo ndani yake ilikuwa na nyimbo kama vile "Nyumba Yangu", "Lipua" na nyenginezo. Mechanism walifanya kati ya 2015 na 2016. Wakati Fasihi Simulizi wamefanya kwenye 2016 mwishoni.

Albamu za wanachama na nyimbo maarufu[hariri | hariri chanzo]

Adam Shule Kongwe wa mbele kabisa na DDC wakiwa katika seti ya kutayarisha video ya "Mazishi".

Mwaka wa 2017, DDC walisimama kama kundi, lakini walikuwa wasimamia albamu za wanakundi wenzao ambao ni Adam Shule Kongwe na Javan na EP ya Andre K iliyooitwa Elimu ya Juu. EP ya A-K ilikuwa na nyimbo nne, na albamu ya kina Adam ilikuwa na nyimbo kama 17 hivi, CK au "Chini Kabisa". Pamoja na kufanya ngoma kibao wana DDC, wimbo ambao ulizua gumzo kwa wananchi na kuanza kuelewa harakati zao ni "Naelekea Ikulu". Hilo lilisababishwa na kutolewa kipindi mwafaka ambapo harakati za uchaguzi mkuu wa Tanzania, 2015. Wimbo ulipendwa sana kwa sababu tu ulizungumzia harakati hizo-hizo kwa kipindi hicho. Pamoja na hayo, uandishi wa wimbo ulikuwa wa kipekee sana. Isitoshe, wimbo ulikuwa unazungumzia matatizo ya serikali na wananchi wake. Bado wengi walitaka kujua kilichomo ndani kwa sababu hawakujuwa nani kaimbwa ndani hadi uusikie. Vilevile wimbo wa "Shabiki" nao ulipendwa. Wimbo uliangalia hali halisi ya mashabki wa hip hop jinsi wanavyounga mkono harakati za hip hop mtandaoni lakini kazi za wasanii wanao waunga mkono hawanunui. Njia pekee ya kumwezesha msanii aendelee kukupa burudani unayoipata ni kununua kazi zao. Wimbo ulitazama sana jinsi shabiki anavyofeli katika vitendo na hasa ulimnanga shabiki bandia.

Nyimbo zote za juu zimetayarishwa na Duke na zinapatikana katika albamu ya "the Element Vol. II". Wimbo mwingine uliotingisha kutoka DDC ni "Cha Juu" wa Andre K. uliangalia sana harakati za kitaa. Hasa ulitazama ugumu wa maisha mtaani, vurugu, usalama na hali halisi ya maisha ya uswahilini yalivyo. Utoaji wa nyimbo hizi ulikuwa hauzidi siku mbili tangu kutoka wimbo wa kwanza. Yaani, leo huu, kesho kutwa huu na nyinginezo zikafuata. Ngoma nyengine inaitwa Katiba walifanya na Sugu, hiyo nayo ilibamba kinoma. Hasa ilitazama msanii katika kusimamia katiba. Wimbo ulitamba na wengi walisikia balaa la Sugu ndani ya wimbo. Ukizingatia Sugu na Duke wote wana wapenzi wengi hivyo kusikika sauti na mikono yao katika ngoma hiyo ilisukuma sana kutambalika kwa DDC. Ngoma nyingine zilizotamba ni pamoja na Mazishi na Mitambao, Cola Mdundo, na nyingine kibwena.

Wanachama wa DDC[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha kamili ya wanachama wa DDC;

  1. Adam Shule Skongwe
  2. Andre K (R.I.P)
  3. Miracle
  4. Therapist
  5. Kanja
  6. Slogan
  7. Goda mc
  8. Bad Jahidina
  9. K2da
  10. Javan Chuna Ngozi
  11. Hafee
  12. Gilson
  13. Sali Trejo

Albamu za DDC[hariri | hariri chanzo]

Albamu walizotoa kama kundi, bila msanii mmoja kutoka katika kundi mpaka sasa ni tatu.
Nazo:

  1. The Element Vol. II (2014)
  2. Mechanism (2015)
  3. Fasihi Simulizi (2016)
  4. Dira (2020)

Albamu za wanachama[hariri | hariri chanzo]

  1. Chini Kabisa - Adam Shule Kongwe na Javan Chuna (2017)
  2. Elimu ya Juu EP (Andre K).
  3. Anko - Adam Shule Kongwe (2018)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]