Nenda kwa yaliyomo

Djelimady Tounkara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Djelimady Tounkara ni mwanamuziki wa nchini Mali na mmoja wa wapiga gitaa maarufu Barani Afrika.

Maisha na Kazi

[hariri | hariri chanzo]

Tounkara alizaliwa magharibi mwa mji mkuu wa Mali, Bamako. Wakati alipohamia mji mkuu wa Mali, Bamako mwaka 1960, alikuwa amepanga kufanya kazi kama fundi nguo. Lakini muziki ulikuwa wito wenye nguvu. Alianza kupiga gitaa katika bendi kubwa ya mtaani iliyofadhiliwa na serikali, Orchestre Misira. Djelimady alipiga gitaa vizuri zaidi katika bendi na alichaguliwa kujiunga na mpiga gitaa wa Orchestre National kama mpiga gitaa wa rhythm na kupewa heshima kubwa kama mpiga gitaa mdogo.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Djelimady Tounkara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.