Dilek Koçbay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dilek Koçbay mnamo 2014

Dilek Koçbay (alizaliwa Desemba 30, 1982), ni mwamuzi wa mpira wa miguu wa Uturuki aliyeorodheshwa kwenye orodha ya waamuzi wanawake wa FIFA.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa huko Balıkesir, Uturuki. Baba yake Mehmet Özdemir alikuwa mwamuzi wa mpira wa miguu, ambaye alimpa hamasa katika kazi ya uamuzi.

Alisomea elimu ya mzaoezi ya viungo na michezo katika Chuo kikuu cha Balıkesir, na kuwa mwalimu baada ya kuhitimu. Ameolewa na Zafer Koçbay, mwamuzi wa zamani wa mpira wa miguu. [1]Wanaishi Çanakkale.[2]

Kazi ya uamuzi[hariri | hariri chanzo]

Koçbay alianza kazi yake ya uamuzi rasmi kama mwamuzi msaidizi katika mechi ya Ligi daraja la Tatu ya TFF mnamo Oktoba 20, 2007.[3]

Mnamo Septemba 2012, alichezesha mechi ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 19 ya Uturuki na Wales iliyochezwa nchini Uturuki.

Koçbay aliwahi kuwa mwamuzi katika mashindano ya kufuzu UEFA ya wanawake chini miaka 17 mwaka 2014.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "ZAFER KOÇBAY DA BIRAKTI". web.archive.org. 2014-12-17. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-17. Iliwekwa mnamo 2023-04-06. 
  2. "Kim Demiş “Kadından Hakem Olmaz” Diye?". www.canakkaletravel.com (kwa Kituruki). Iliwekwa mnamo 2023-04-06. 
  3. "DİLEK KOÇBAY - Hakem Bilgileri TFF". www.tff.org. Iliwekwa mnamo 2023-04-06. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dilek Koçbay kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.