Deo Kanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Deo Kanda
Youth career
2005–2007Jack Trésor FC
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2007–2009DC Motema Pembe2(0)
2009–2013TP Mazembe40(15)
2013–2014Raja Casablanca3(0)
2014–2015AS Vita Club2(1)
2015AEL0(0)
2015–TP Mazembe
Timu ya Taifa ya Kandanda
2011–DR Congo21(4)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 01:05, 15 July 2013 (UTC).

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 01:05, 15 July 2013 (UTC)

Deo Kanda A Mukok (amezaliwa 11 Agosti 1989) ni mchezaji wa soka raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayecheza kama mshambuliaji katika klabu ya Simba S.C. nchini Tanzania.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Akiwa mzaliwa wa Matadi, Deo Kanda alianza maisha ya Soka katika klabu ya Jack Trésor FC.[1] Ali saini mkataba wake wa soka la kulipwa na klabu kutokea Kinshasa ya DC Motema Pembe.[2]

Baadaye alihamia kwa wapinzani wa jadi klabu ya TP Mazembe mnamo mwaka 2009, alifanikiwa kucheza fainali za kombe la dunia ngazi ya klabu kwa misimu ya 2009 na 2010, katika mechi ya fainali walipoteza kwa goli 3-0 dhidi ya Internazionale.[3]

Katika fainali za klabu bingwa afrika, alifunga goli la muhimu sana lililowafanya Mazembe kushinda taji hilo.[4]

Mnamo Aprili 2013, alifanya majaribio na klabu ya Misri Al Ahly,[5] hata na hivyo hakusajiliwa na klabu hiyo. Juli 2013 alijiunga na klabu ya nchini Morocco, Raja Casablanca, na kusaini mkataba wa miaka mitatu.[6]

Katika timu ya taifa Déo Kanda kafanikiwa kucheza mechi mbili tu katika mashindano ya kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Déo Kanda, un flanc gauche offensif (French). La Capitale (29 October 2011).
  2. Tungila, Serge (7 May 2007). Deo Kanda (French). Congofoot. Jalada kutoka ya awali juu ya 27 May 2007.
  3. Inter Milan beat TP Mazembe to take World Club crown. BBC Sport (2010-12-18). Iliwekwa mnamo 2010-12-19.
  4. McAnally, Nicholas (14 November 2010). Deo Kanda : "Un rêve devenu réalité" (French). Afrik.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-08-13. Iliwekwa mnamo 2019-11-01.
  5. Devils continue to eye Kanda. Tarek Talaat. SuperSport (2013-04-24). Iliwekwa mnamo 2013-07-15.
  6. DR Congo international Déo Kanda concludes three-year deal with Raja Casablanca. Ngoh Divine. Starafrica.com (2013-07-12). Jalada kutoka ya awali juu ya 4 March 2016. Iliwekwa mnamo 2013-07-15.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]