David Mwiraria
David (Daudi) Mwiraria (3 Septemba 1938 - 13 Aprili 2017) alikuwa Waziri wa Mazingira na Maliasili na awali alikuwa Waziri wa Fedha wa Kenya hadi Desemba 2007 wakati Kenya ilifanya Uchaguzi mkuu. Licha ya kugombea tena kwa tikiti ya Party of National Unity, alishindwa kukihifadhi kiti chake kama Mbunge wa North Imenti dhidi ya Silas Muriuki, ambaye alikuwa akitumia tikiti ya Mazingira Green Party of Kenya.
Kufuatia ishara kwamba alikuwa amehusika katika Kashfa ya Anglo leasing, aliamua kujiuzulu kama Waziri wa Fedha tarehe 1 Februari 2006 [1] Alisisitiza kwamba alikuwa hana hatia na kuwa alijiuzulu ili uchunguzi ufanywe.[2] Hata kama hakukuwa na ripoti ya uchunguzi ya kumwondolea Mwiraria mashtaka, Rais Mwai Kibaki alimteua kama Waziri wa Mazingira tarehe 24 Julai 2007.
Alipata shahada yake ya juu katika Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda mwaka 1966 (kisha sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki).
Mwiraria yupo katika kanda zilizotolewa kwenye intaneti mwaka 2006 na John Githongo, mfukuzwa wa nchi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa katika Serikali ya Kenya, ambazo zinaonyesha Mwiraria alikuwa anajaribu kumzuia Githongo kuuliza maswali kuhusu wizi wa zaidi ya dola milioni 777 katika mfululizo wa mikataba 18 ya iliyohusiana na usalama, pia huitwa kashfa ya Anglo leasing.
Mnamo Desemba 2007, Mwiraria, Nicholas Biwott, Sanjay Kumar Ramniklal, na Manoj Ramniklal Panacha Shah walipigwa marufuku ya kusafiri au kupitia Uingereza kutokana na mashtaka ya rushwa.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kenyan Finance Minister Resigns Following Corruption Allegations", VOA News, Voice of America, 1 Februari 2008. Retrieved on 25 Desemba 2008.
- ↑ "Waziri wa Kenya wa 'ufisadi' ajiuzulu", BBC News, 1 Februari 2006.
- ↑ "Uingereza kupiga marufuku kusafiri kwa mawaziri wa Kenya", BBC News, 21 Desemba 2007.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.parliament.go.ke/MPs/members_mwiraria_d.php Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- http://www.marsgroupkenya.org/pages/clips/Mwiraria-Githongo.php Ilihifadhiwa 9 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanasiasa huyu wa Kenya bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |