Daniel Ebenyo
Daniel Simiu Ebenyo (alizaliwa 18 Septemba 1995) ni mwanariadha wa mbio za kati kutoka nchini Kenya[1].
Alitoka Baragoi, kaunti ya Samburu, baada ya kumpoteza baba yake katika maisha yake ya awali katika ajali aliyoipata akiwa na mifugo yao, alilelewa na mama yake na baadae bibi yake[2].Alitokea na kusema kuwa ni kilomita 24 kila siku kutoka nyumbani kwenda shuleni,shule ya sekondari ya Aiyam ndiko kuliko mfanya kuwa mwanariadha mzuri hivi sasa,kwa kuwa njia aliyokuwa akipita kuelekea shule ilikuwa mbaya na hatari hivyo ilimfanya kuweza kutembea umbali huo mrefu kwa muda mfupi akitoka asubuhi ili kuweza kuwahi vipindi vyake vya shuleni.
Alimaliza katika nafasi ya pili katika majaribio ya mashindano ya dunia ya kitaifa ya Kenya 2019[3]. Japokuwa alishindwa kumaliza mashindano yale, kwakua alishindwa kuwa na vigezo vya Riadha kutoka shirika la riadha liitwalo Athletes Integrity Unit (AIU).[4]Simiyu alipitia majaribio ya kuweza kujiunga na mashindano mara kadhaa lakini alishindwa kupita katika vigezo vikuu vitatu ambavyo ni vya lazima kuvifikia mchezaji yeyote kabla ya kuanza mashindano hayo,ikiwemo kipimo cha mkojo na damu. Simiyu ali lilaumu shirika la riadha la kenya kwa kuto kumtaarifu mapema kuhusu vigezo hivyo kabla ya yeye kusaini majaribio hayo[5]. Alivunjika moyo sana na kutishia kuacha mashindano hayo,na kwenda kujiunga na mashindano ya magari,na alishinda Safaricom Kisii ya kilomita 10 katika muda wa dakika 29:16.71 ,na pia kilomita 10 katika mashindano ya Nairobi Marathon katika rekodi ya muda wa dakika 28:23[6].
Alianza msimu wake wa mwaka 2021 na ushindi wa elite-only San Silvestre Vallecana wa kilomita 10 nchini hispania mnamo tarehe 3 ya Januari[7].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Daniel Simiu EBENYO | Profile | World Athletics". worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
- ↑ Enda (2019-04-09). "A peek into the lives of Enda athletes". Medium (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
- ↑ Timothy Olobulu (2021-06-19). "Conseslus, Timothy Cheruiyot out as Kenya names team for Tokyo Olympics". Capital Sports (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
- ↑ "Kenyan duo barred from Doha after failing to meet anti-doping rules", Reuters (kwa Kiingereza), 2019-09-24, iliwekwa mnamo 2021-09-27
- ↑ "Simiyu finding it hard to train alone but optimistic for future". People Daily (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2020-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
- ↑ https://www.the-star.co.ke/authors/agichana. "Disappointed Simiyu contemplates switching top roads". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
{{cite web}}
: External link in
(help)|author=
- ↑ Sentinel Digital Desk (2021-01-09). "Kenya's Daniel Simiu Ebenyo eyes first medal this season - Sentinelassam". www.sentinelassam.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Daniel Ebenyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |