Cynthia Munwangari
Cynthia Munwangari | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Cynthia Munwangari |
Alizaliwa | 8 Septemba 1990 |
Nchi | Burundi |
Kazi yake | Mwanamitindo |
Tovuti rasmi | Cy’Mun Collection". |
Cynthia Munwangari (amezaliwa Bujumbura. 8 Septemba 1990) ni mbunifu wa mitindo, mwanamitindo na mfanyabiashara wa nchini Burundi. Yeye ndiye mwanzilishi na mkurugenzi wa sasa wa "Bujumbura Fashion Week", inayofanyika kila mwaka mjini Bujumbura (jiji kubwa zaidi nchini humo).[1]
Historia na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Amezaliwa huko Bujumbura, mji mkubwa na mji mkuu wa Burundi. Baba yake ni raia wa Burundi na mama yake ni wa Rwanda. [1] Yeye ni mtoto wa tatu na ana kaka wawili na dada mmoja. Alipata elimu yake yote nchini Burundi. [1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Munwangari ndiye mwanzilishi na mmiliki wa lebo ya mavazi ya "Cy’Mun Collection". Yeye pia ni mwanamitindo wa lebo yake. [1]Mnamo Julai 2014, Cynthia Munwangari, akiwa na umri wa miaka 23 aliandaa Wiki ya Mitindo ya kwanza ya Bujumbura kuhudhuriwa na wabunifu 24 wa Kiafrika, kutoka nchi 14. Gwaride la mitindo la saa nne lilijumuisha wanamitindo arobaini na lilihudhuriwa na Pierre Nkurunziza, rais wa Burundi. [2] [3] [4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 https://en.m.wikipedia.org/wiki/Cynthia_Munwangari#cite_ref-Her_1-3
- ↑ "Cynthia Munwangari", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-01-02, iliwekwa mnamo 2022-03-18
- ↑ "Cynthia Munwangari", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-01-02, iliwekwa mnamo 2022-03-18
- ↑ "Daily Monitor", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-02-26, iliwekwa mnamo 2022-03-18