Chumba cha mazoezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Watu wakifanya mazoezi katika Chumba cha mazoezi

Chumba cha mazoezi (kwa lugha ya Kiingereza: gym, kifupisho cha neno "gymnasium" ) ni mahala palipotengwa kwa kufanyia mazoezi ya kimwili. Chumba hiki huwa na karakana za kuongeza misuli kama vile vyuma vizito, tredimili na kamba za kurukia.

Vyumba vya namna hiyo hupatikana haswa kwa wanaspoti wa mchezo wa kushindana nguvu na watimua misuli.

Vyumba hivyo hulipiwa ambapo mtu anayetaka kushiriki katika mazoezi kwa chumba fulani hulipa ada. Hata hivyo, huenda ukaanza gym nyumbani kwako kwa kununua vifaa vya mazoezi na kutenga chumba au mahala fulani kwa kufanyia mazoezi.

Historia ya chumba cha mazoezi[hariri | hariri chanzo]

Vyumba vya kwanza vya mazoezi vilipatikana nchini Persia miaka 3000 iliyopita.

Bafu za Waroma wa Kale pia zilikuwa na vyombo vya mazoezi na kwa kuta mlikuwa na michoro ya mabingwa wa spoti.

Vyumba vya mazoezi vya kisasa[hariri | hariri chanzo]

Hivi leo, vyumba vya mazoezi vipo kwa wingi na wateja wake huwa watu wanaotaka kupunguza uzani au kupata umbo fulani wakipoteza ufuta wa mwili. Huwa na mwalimu wa kuwahudumia ambaye huwa amesomea masomo ya mazoezi ili wajue mazoezi yanayomfaa mtu fulani mwenye uzani fulani na anayetaka kupunguza ufuta kwa muda fulani. Wateja hulipa kwa mwezi au kila siku.

Huwa kuna karakana za kufanya mazoezi ingawa mazoezi mengine si lazima yafanywe kwa karakana zile.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chumba cha mazoezi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.