Tredimili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tredimili (kutoka Kiingereza "treadmill") ni kifaa kinachopatikana katika chumba cha kufanyia mazoezi (gym) ambacho hutumiwa kwa kutembelea pahala pamoja ili mtu aweze kupunguza kilo mwilini.

Tredimili hutengenezwa kwa kutumia kamba au uzio ambao huzungukazunguka huku mtu akitembea juu. Kwa hali hii, mtu huhisi kana kwamba ametembea maili nyingi na kutoa jasho ilhali yu palepale.

Tredimili hutumia nishati ya stima ili iweze kuzungushazungusha ule uzio.

Historia ya tredimili[hariri | hariri chanzo]

Kitambo, tredimili zilitumika kwa kusaga mtama na mahindi ambapo nguvu zile za kukanyagia ule uzio zilitumika kuzungusha kisiagi na kwa hiyo kufanya mahindi au mtama viwe unga.

Vile vile, tredimili au trediwhili kama inavyojulikana ilitumika kwa kuwatesa wafungwa waliokosa nidhamu. Kwa kutembezwa katika ule uzio unaozungukazunguka, wafungwa walihisi maonevu na kuchoka na kwa hiyo hawangekosa nidhamu tena.

Matumizi ya tredimili leo[hariri | hariri chanzo]

Hivi leo, tredimili imekuwepo katika kila chumba cha mazoezi. Takwimu[1][2] zaonyesha kwamba tredimili zinanunuliwa kwa wingi sana.

Tredimili zina uzani tofauti. Kuna zile ambazo hufai kuzitumia kama wewe umefikisha uzani wa paundi mia nne kwenda juu. Kuna nyingine za uzani wa paundi mia tatu hamsini kwenda juu. Hivyo kuna tredimili tofauti kulingana na watumiaji. Walio na uzani wa wastani, watatumia tredimili ya wastani huku walio na uzito mwingi watatumia tredimili za watu wakubwa [3].

Mambo mengine ya kuzingatia ni mwendo wa tredimili (kwa maana tredimilli zina mwendo tofauti), ukubwa wake, na mwinuko wake.[4]

Hata hivyo, wanaotaka kupunguza uzani wamekuwa wakitumia vitu vingine kama vile kamba za kurukia, baiskeli ya kwendeshea, madawa [5][6] na mazoezi ukitumia benchi.

Vifaa katika tredimili[hariri | hariri chanzo]

Pindi teknolojia inavyoendelea ndivyo tredimili zinavyopata vifaa tofauti za kuziboresha kama:

  1. Feni ya kupepea ili mwenye kutumia asipatwe na joto jingi
  2. Mahala pa kuwekelea pajatarakilishi ili mtumizi aweze kufanya kazi huku akitembea kwa tredimili
  3. Mahala pa kuweka chaji kwa simu
  4. Spika ili mtembeaji aweze kusikiza muziki anapofanya mazoezi.

Usalama ukitumia tredimili[hariri | hariri chanzo]

Uzio wa tredimili huenda ukakuangusha na ukaumia vibaya. Pindi tredimili inapozunguka, inafaa ukimbie. Vitu kama utumizi wa simu ya rununu, unywaji wa kahawa huenda zikakufanya usahau kwamba upo juu ya tredimili, ukaenda pole na kuumia vibaya maana uzio wa mashine huu hautasimama.

Viatu vya tredimili vyafaa viwe vya kispoti; huwezi ukatumia tredimili na viatu vya ofisini kufanyia mazoezi[7].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tredimili kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.