Chela
Chela ni kata ya Wilaya ya Msalala katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 31,991 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 20,760 waishio humo.[2]
Katika mlima Chela kuna chemchemi ya Kwa mfufumo ambapo wenyeji huenda kufanya shughuli za kimila. Inaaminiwa nao kuwa ukifika una damu nzuri maji meupe yanatoka, ngoma na vigelegele. Lakini ukiwa una damu mbaya yale maji yanageuka kuwa funza au tope zito au damu. Wakati huo unatakiwa uondoke haraka sana.
Hiyo chemchemi inamwaga maji yake kwenye bwawa lililoko Chela senta. Maji hayo waliyatengenezea miundombinu ya bomba ili wawe wanayauza lakini yaligoma kutoka mpaka walipoamuru yachotwe bure, hapo yakaanza kutoka mpaka leo. Kuna samaki ukimkamata pale ukimpika saivi mpaka watelemke bwawa la chini ndipo ukiwavua wanaiva wakipikwa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Msalala - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania | ||||
---|---|---|---|---|
Bugarama | Bulige | Bulyan'hulu | Busangi | Chela | Ikinda | Isaka | Jana | Kashishi | Lunguya | Mega | Mwakata | Mwalugulu | Mwanase | Ngaya | Ntobo | Segese | Shilela
|