Nenda kwa yaliyomo

Chanjo ya malaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chanjo ya malaria ni kati ya zile muhimu zaidi, kutokana na wingi wa waathirika.

Tarehe 6 Oktoba 2021, wahusika wa Shirika la Afya Duniani (WHO) walitangaza kwamba wao wanapendekeza chanjo ya malaria inayoitwa RTS,S/ASO1 au Mosquirix kwa watoto wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara. Wanapendekeza chanjo kwa watoto wanaoishi maeneo yenye maambukizi makubwa ya "P. falciparum" wa malaria. Tangazo hili ni hatua ya kwanza kwa usambazaji wa chanjo kwa nchi za Afrika. [1]

Sasa, chanjo ya malaria inajaribiwa kwa jaribio la kliniki katika nchi za Ghana, Kenya, na Malawi. Jaribio hilo limeanza mwaka 2019 na hadi wakati huo, watoto 800,000 wamepata chanjo ya malaria.

Mkurugenzi wa WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreysus alisema, "Kutumia chanjo hii pamoja na zana zilizopo kwa kuzuia malaria kutaokoa uhai wa watu elfu kumi kila mwaka".[2] Mwaka wa kwanza chanjo ya malaria ilipotumika ilikuwa wa ufanisi wa asilimia 50 kwa kuzuia kesi za malaria kali. Baada ya miaka miwili, ilikuwa na ufanisi wa karibu asilimia 80! Jumla Mosquirix itapunguza kesi za malaria kali kwa asilimia 30. Watoto kuanzia umri wa miezi mitano au zaidi wameanza kupata dozi ya kwanza ya chanjo na watapata dozi kila mwezi kwa mara ya tatu. Basi, watapata dozi ya mwisho baada ya mwezi wa kumi na nane. Dozi ya mwisho ni muhimu kwa sababu itasaidia kuzuia kesi nyingi za Malaria.

Chanjo ya malaria ni maendeleo makubwa! Ni chanjo ya kwanza kwa ugonjwa wa vimelea.

  1. Mandavilli, Apoorva (2021-10-06), "A 'Historic Event': First Malaria Vaccine Approved by W.H.O.", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2021-10-19
  2. "WHO recommends groundbreaking malaria vaccine for children at risk". www.who.int (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-10-19.