Catherine Valentine Magige
Mandhari
Catherine Valentine Magige (alizaliwa mkoani Arusha 8 Mei 1981) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka mitano (2015 – 2020 [1]). Amehitimu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Kimandolu kuanzia 1989-1995 na elimu ya sekondari katika shule wa wasichana Ngarenaro kuanzia 1996-1999.[2].
Mwaka 2014 alikuwa mwakilishi katika bunge la Katiba [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/wasifu-wa-ndani-mh-catherine-magige-na-nia-yake-ya-2015.290791/
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/wasifu-wa-ndani-mh-catherine-magige-na-nia-yake-ya-2015.290791/
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |