Carole Gray

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Carole Gray (kuzaliwa Bulawayo, Zimbabwe, 1938[1]) alikuwa mcheza dansi na mwigizaji wa filamu na maonyesho ya jukwaani ambaye katika kazi yake hapo awali alianzia nchini Uingereza na alijulikana sana kwa uhusika wake katika muziki wa jumba la Sanaa la West End miaka ya 1960.

Alizaliwa Rhodesia Kusini, akafika nchini Uingereza mwaka 1956, na kuanza kazi yake ya uigizaji kwa miaka 12, alionekana katika filamu mbalimbali mojawapo iliyompatia umaarufu ni filamu ya The Avengers, lakini filamu iliyomtambulisha ni ya mchumba wake Cliff Richard, bibie Toni kwa jina la The Young Ones ya mwaka 1961.

Baada ya hapo, alijitokeza katika filamu nyingine tofauti hususani filamu za kutisha kama vile, Curse of the Fly, Devils of Darkness, na Island of Terror, na alipewa jina la utani la "Scream Queen".[2] Mnamo mwaka 1968, alirudi nyumbani Afrika ambapo alishiriki katika maonyesho ya jukwaani kama Harvey]], mwaka 1968, Fiddler on the Roof, mwaka 1969, na maonyesho ya Taubie Kushlick ya ‘’No, No, Nanette’’ katika ukumbi wa Alexander Theatre, Johannesburg, mwaka 1972.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Carole aliolewa na mume wake wa kwanza Graham Du Toit, mnamo Disemba 1957. Walipotalakiana, ndoa yake ya pili ilikuwa na Douglas Cullinan, mfanyabiashara wa almasi.

Sehemu ya Sanaa[hariri | hariri chanzo]

  • The Prince and the Showgirl (1957) – Mcheza densi
  • The Young Ones (1961) - Toni
  • Rattle of a Simple Man (1964) – Nesi wa hospitali ya wilaya
  • Devils of Darkness (1965) - Tania
  • Curse of the Fly (1965) - Patricia Stanley
  • Duel at Sundown (1965) - Nancy Greenwood
  • Island of Terror (1966) - Toni Merrill
  • The Brides of Fu Manchu (1966) - Michel Merlin
  • Oh! What a Lovely War (1969) – muimbaji wa kiitikio

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carole Gray kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.