Nenda kwa yaliyomo

Carlos Slim Helu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Carlos Helu
Carlos Helu (2010)

Carlos Slim Helú (matamshi ya Kihispania: [kaɾlos eslim elu]; alizaliwa 28 Januari 1940) ni mhandisi, mwekezaji na mtaalamu wa biashara wa Mexiko. Yeye ni mtu tajiri zaidi nchini.

Kuanzia 2010 hadi 2013, Slim aliwekwa nafasi ya kuwa mtu tajiri zaidi duniani kadiri ya gazeti la biashara la Forbes.

Alipata bahati yake kutokana na umiliki wake mkubwa wa idadi ya kampuni za Mexiko kupitia kikundi chake, Grupo Carso. Kuanzia Juni 2018 ni mtu tajiri wa saba ulimwenguni, kwa mujibu wa orodha ya Forbes ya Mabilionea wa Dunia, akiwa na wastani wa thamani $ 61.3 bilioni.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carlos Slim Helu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.