Carlos Agostinho do Rosário

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Carlos Agostinho do Rosário (amezaliwa 26 Oktoba 1954) ni mwanasiasa wa Msumbiji ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Msumbiji tangu tarehe 17 Januari 2015. Yeye ni mwanachama wa FRELIMO na anahudumu chini ya Rais Filipe Nyusi.

Alifanya kazi kama mtumishi wa umma mnamo miaka ya 1970 na alikuwa Gavana wa Mkoa wa Zambezia kati ya mwaka wa 1987 na 1994. Baadaye alihudumu kwa muda mfupi kama mbunge mnamo 1994 kabla ya kuwa Waziri wa Kilimo na Uvuvi, ambaye kwa muda huo alihudumu hadi 1999. Baadaye alikuwa Waziri mwanadiplomasia huko Asia; kabla ya kuteuliwa kama Waziri Mkuu, Rosario aliwahi kuwa Balozi nchini Indonesia.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carlos Agostinho do Rosário kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.