Nenda kwa yaliyomo

Shirika la Mkombozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka CSSR)
Mt. Alfonso Maria wa Liguori (1696-1787), Mwanzilishi wa shirika.
Mt. Yohane Nepomuk Neumann (1811-1860), askofu wa kwanza wa Marekani kutangazwa mtakatifu.

Shirika la Mkombozi Mtakatifu sana (kwa Kilatini: Congregatio Sanctissimi Redemptoris – Ufupisho: C.Ss.R au CSSR) ni shirika la kitawa la kimisionari la Kanisa Katoliki lililoanzishwa na Alfonso Maria wa Liguori tarehe 9 Novemba 1732 huko Scala (karibu na Amalfi, Italia) ili kushughulikia watu waliosahaulika wa mkoa wa Napoli.

Kwa Kiingereza wanashirika wanajulikana kama Redemptorists. Wakiwa mapadri na mabradha wanafanya kazi katika nchi zaidi ya 77 duniani kote. Mkuu wao anaitwa Michael Brehl.

Wanashirika maarufu

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shirika la Mkombozi kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.