Nenda kwa yaliyomo

Bwiru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bwiru
Jike la bwiru koo-jeusi
Jike la bwiru koo-jeusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Platysteiridae (Ndege walio na mnasaba na bwiru)
Jenasi: Platysteira
Jardine & Selby, 1830
Spishi: Angalia katiba.

Bwiru ni ndege wadogo wa jenasi Platysteira katika familia Platysteiridae wanaotokea Afrika chini ya Sahara. Zamani waliainishwa katika familia Muscicapidae. Ndege hawa wana ngozi tupu nyekundu au buluu juu ya au pande zote za macho. Kwa kawaida ni weusi juu na weupe chini na wana mlia mweusi kidarini. Mara nyingi dume ana koo jeupe na jike koo jeusi au kahawia. Hula wadudu na hulijenga tago lao kwa uvumwani na utando wa buibui kwa umbo wa kikombe katika mti au kichaka. Jike huyataga mayai 2-4.