Bruno Tshibala
Mandhari
Bruno Tshibala Nzenze (alizaliwa 20 Februari 1956) ni mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo tangu Mei 2017.
Alianza harakati za kisiasa wakati akiwa mwanafunzi mwezi Aprili 1980 akiwa na umri wa miaka 25 alipoingia chama cha siasa cha Zaire wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko.
Mnamo Desemba 1980, yeye na wabunge kumi na tatu waliandika barua ya kumuomba Rais Mobutu mageuzi ya kidemokrasia wakati nchi ilikuwa bado chini ya mfumo wa chama kimoja.
Tarehe 7 Aprili 2017, Rais Joseph Kabila alimteua kuwa Waziri Mkuu na alianza kazi rasmi tarehe 18 Mei 2017.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bruno Tshibala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |