Bromi
Mandhari
(Elekezwa kutoka Bromini)
Bromi | |
---|---|
Jina la Elementi | Bromi |
Alama | Br |
Namba atomia | 35 |
Mfululizo safu | Halojeni |
Uzani atomia | 79.904 |
Valensi | 2, 8, 18, 7 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 265.8 K (-7.3 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 332.0 K (58.8 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 6 · 104 % |
Hali maada | kiowevu |
Bromi (pia bromini, kut. Kigiriki βρῶμος bromos "kunuka kwa wanyama" ) ni elementi yenye namba atomia 35 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 35. Uzani atomia ni 79.904 na alama yake ni Br. Ni elementi ya tatu katika safu ya halojeni.
Katika hali sanifu ni kiowevu yenye rangi nyekundu kahawia. Inamenyuka haraka na elementi nyingine na kwa wanyama pia watu ni sumu.
Bromi yapatikana kwa wingi katika maji ya bahari.
-
Bromi ya kiowevu ndani ya testitubu. Juu ya kiowevu iko gesi ya bromi.