Bohemian Rhapsody
Bohemian Rhapsody ni wimbo wa bendi ya Rock ya Uingereza Queen. Ilitungwa na Freddie Mercury ikatolewa kwenye albamu yao ya mwaka 1975 A Night at the Opera.
Muundo
[hariri | hariri chanzo]Bohemian Rhapsody ina sehemu sita:[1]
1. Ufunguzi (0:00–0:49) – 14 % 2. Wimbo la masimulizi (0:49–2:37) – 31 % 3. Solo ya gitaa (2:37–3:03) – 7 %4. Mwigo wa kubeza opera (3:03–4:08) – 18 % 5. Muziki wa rock kali (4:08–4:55) – 13 % 6. Kufunga kitulivu (4:56–5:55) – 17 %
Video
[hariri | hariri chanzo]Kampuni ya EMI iliyotoa albamu ilikuwa na wasiwasi juu ya wimbo ikaona afadhali kutengeneza video ili kuongeza umaarufu wake. Wimbo pamoja na video zilifanykiwa sana na kuwa kielelezo kwa kawaida ya baadaye ya kutangaza nyimbo na bendi kwa njia ya video.[2]
Mafanikio kwenye chati
[hariri | hariri chanzo]Mwanzoni kampuni ya rekodi ilikuwa na wasiwasi kama wimbo huo utapokewa kwenye vituo vya redio kwa sababu ya urefu wake (dakika 5 na sekunde 55) na muundo wake uliokuwa tata ukilinganishwa na nyimbo za siku zile[3]. Walifanya majaribio kwa kuitoa awali kwa kituo cha redio ya Capital Radio; katika wikendi moja ilisikika mara 14 na wasikilizaji walipenda sana[4]. Baadaye ikawa #1 kwenye chati nyingi. [5] Sasa inachezwa kwenye redio kwa urefu kamili.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Bohemian Rhapsody, tovuti ya queensongs.info
- ↑ Muikku, Jari (1990). "On the role and tasks of a record producer". Popular Music and Society. 14 (1): 25–33. doi:10.1080/03007769008591381.
- ↑ "Bohemian rhapsody celebrates 40 years: 19 things you didn't know about the queen anthem", 30 October 2015.
- ↑ https://www.nytimes.com/2005/12/27/arts/music/unconventional-queen-hit-still-rocks-after-30-years.html Chiu, David (27 December 2005). "Unconventional Queen Hit Still Rocks After 30 Years". The New York Times. Retrieved 12 April 2010.
- ↑ "An Invitation To The Opera." Sound On Sound (October 1995). Retrieved on 2008-11-01.