Bohemia
Mandhari
(Elekezwa kutoka Boemia)
Bohemia (kwa Kicheki na Kislovakia: Čechy; kwa Kijerumani: Böhmen; kwa Kipolandi: Czechy) ni mkoa wa kihistoria katika magharibi ya Ucheki.
Jina limetokana na neno la Kilatini kwa ajili ya eneo la kabila la "Boio" ("Boiohaemum" = eneo la Waboio, baadaye: "Bohemia") lililowahi kukalia sehemu zile zamani za Roma ya Kale.
Pamoja na Moravia eneo la Bohemia ni sehemu muhimu ya Ucheki ambayo ni nchi iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya Slovakia kutoka katika Chekoslovakia. Bohemia imepakana na Poland upande wa kaskazini, Ujerumani upande wa kaskazini na magharibi, Austria upande wa Kusini na mkoa wa Moravia upande wa mashariki.
Mji mkuu wa Bohemia ni Praha (kwa Kiingereza: Prague), ambao ni pia mji mkuu wa taifa.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bohemia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |