Boeing F-15 Eagle
Boeing F-15 Eagle ni ndege ya Marekani yenye injini mbili, yenye uwezo wa kupambana kwenye hali zote za hewa iliyotengenezwa na kampuni iitwayo McDonnell Douglas (sasa inajulikana kama Boeing) ya huko nchini Marekani.
Ndege hii imeundwa maalumu kwa ajili ya mapambano ya anga. Aina hii ya ndege ilichaguliwa na jeshi la Marekani itumike kama ndege yao ya vita mwaka 1967.
Pia imeendelea kutumika kama ndege ya kivita na nchi nyingine kama vile Israeli, Saudi Arabia n.k.