Big Show

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Big Show

Huyu ni Big Show akiwa ulingoni
Amezaliwa 8 Februari 1972
Marekani
Kazi yake mpiganaji wa mieleka na muigizaji wa Marekani

Paul Donald Wight II(anajulikana kwa jina la Big Show; alizaliwa 8 Februari 1972) ni mpiganaji wa mieleka na muigizaji wa Marekani, amesajiliwa kwenye kampuni ya WWE, ambapo anafanya kazi kwenye lebo ya Raw.

Big Show aliingia katika Mashindano ya World Championship Wrestling (WCW), ambapo alijulikana kwa jina la The Giant. Mnamo mwaka wa 1999 alisaini mkataba na Shirikisho la mieleka ulimwenguni (WWF).

Katika WWF/WWE na WCW yeye ni bingwa wa saba wa dunia, akiwa ameshikilia mataji ya WCW World Heavyweight Championship mara mbili, WWF/WWE mara mbili, WWE World Heavyweight Championship mara mbili na ECW World Heavyweight Championship mara moja, na huyu ndiye mtu pekee aliyeshikilia mataji manne.

Big Show mwaka 2018.

Nje ya kuwa mpiganaji,Wight ameshiriki katika filamu na vipindi vya televisheni kama Jingle All the Way,The Waterboy,Star Trek Enterprise.Mnamo mwaka 2010 alikuwa na jukumu la kuongoza katika filamu ya uchekeshaji Knucklehead ambayo ilitolewa na WWE Studio.

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Big Show kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.