Nenda kwa yaliyomo

Bertha Egnos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bertha Egnos
Amezaliwa
johannesubrg
Kazi yake mwanamuziki

Bertha Egnos (1 Januari 1913 mpaka 2 Julai 2003) alikuwa ni mwanamuziki wa Afrika Kusini, mwongozaji na mtunzi wa muziki wa theatre kwa maarufu anajulikana kama mgunduzi na muongozaji wa Ipi Tombi.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Bertha "BeBe" Egnos alizaliwa na kukulia katika familia ya Kiyahudi katika kitongoji cha Johannesburg. Alikuwa mwanamuziki kila mara, na aliacha shule akiwa kijana mdogo na kuanza kucheza piano katika kikundi cha maonyesho. Karibu 1934 aliondoka Afrika Kusini na kuanza kuifanyia kaziBBC huko London; pia alisoma piano ya jazba na Reginald Foresythe alipokuwa "Uingereza"na akatengeneza rekodi chache za kwake. [1]


Egnos alirudi Afrika Kusini 1936. Wakati wa Vita vya Pili vya dunia, alianza na kuongoza Bendi ya Drum na Bugle ya wanawake wote. Pia alianza kuandika na kuelekeza revues za muziki wa bembea, na majina yakiwemo Swing 1939 na Swing 1941. Baada ya vita, aliandika vichekesho vya muziki. Miongoni mwa maonyesho yake ni Bo-jungle (1959), Dingaka (1961), Eureka! (1968), na Ipi-Tombi (1974, akiwa na binti yake Gail Lakier. na 1988 “The New Generation” pamoja na mpwa wake Geoffrey Egnos) kulingana na albamu waliyoandika iitwayo "The Warrior," iliyomshirikisha Margaret Singana. [2]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bertha Egnos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.