Berea Park
Ukumbi wa Berea Park ni ukumbi wa michezo ya aina nyingi unaopatikana huko Pretoria, nchini Afrika Kusini, kwenye Mtaa wa Lilian Ngoyi (hapo awali uliojulikana kama Mtaa wa Van der Walt) karibu na mji wa downtown. Imetumika na timu kadhaa za michezo katika mpira wa miguu/soka Berea Park FC ikijumuishwa, pamoja na kriketi ya zamani (Kaskazini Mashariki mwa Transvaa).[1]
Uwanja huo hapo awali ulitumika kama eneo kwa ajili ya kulishia ng’ombe, katika sehemu ya shamba la Hoffman. Mnamo Septemba,mwaka 1882 ulianza kutumiwa kama uwanja wa nyumbani kwa timu ya kriketi ya Pretoria, na ikajulikana kama Berea Park.[2][3]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Septemba mwaka 1882,umbali mdogo kutokea malisho ya zamani ya ng’ombe yalipokua/dakika chache kwa gari la farasi kutoka church square(Mraba wa kanisa) uliwekwa wakfu kama uwanja wa kriketi kwa ajili ya wachezaji wa Pretoria. Ardhi hiyo ilikuwa inamilikiwa na mama mmoja mjane aliyejulikana kwa jina la [[[Hoffman]] na ilikuwa sehemu ya shamba ikiwa ni pamoja na ile ambayo sasa ni Fountains Valley, Pretoria. Wakati Walter wa Uingereza alipotembelea Afrika Kusini mnamo mwaka 1892, uwanja huo ulikuwa tayari unajulikana kama Berea Park.
Timu ya Pretoria ilicheza dhidi ya wageni wa Kiingereza, katika mechi ya kwanza ya kimataifa ya kriketi huko Pretoria, wakati huo mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika Kusini (ZAR). Timu ya Pretoria ilishirikisha wachezaji 22 dhidi ya 11 kwa upande wa Walter Read. Katika mechi hiyo, iliyofanyika Januari 29-30, mwaka1892, timu ya Pretoria ilishinda zamu moja na kushindwa kwa makimbizo 29. Katika msimu wa 1906-07 wa Kombe la Currie uliofanyika Johannesburg na timu ya Pretoria ikiashiria mwanzo wa nyumbani wa kriketi daraja la kwanza, Timu ya kriket iliyojulikana kwa jina la Northerns ilitumia Hifadhi hiyo ya Pretoria kutoka 1937-38 hadi ile ya 1984-85, ambapo uwanja wao mpya wa SuperSport Park au Centurion Park ulipokamilika.
Mnamo mwaka 1897, wafanyakazi walijenga jumba la makutano cha kundi cha kwanza hapo. Gari la kwanza lilionyeshwa Afrika Kusini huko Berea Park mwaka huo huo. Rais Paul Kruger wa ZAR alitoa hotuba kwa hafla hiyo.
Mnamo mwaka 1903, Reli za Afrika Kusini (sasa Transnet) ilinunua sehemu hiyo ya Park kama uwanja wa michezo kwa wafanyikazi wa reli. Nyumba ya makutano ya kikundi ya zamani ya kilabu ikawa ikitumika kama maktaba, chumba cha muziki, na baa. Jumba la kilabu la kusini lilijengwa mnamo mwaka 1907, wakati ile ya kaskazini iliongezwa mnamo mwaka 1926 mwaka ambao Klabu ya mpira ya raga ya Berea ilifunguliwa. Timu ya mpira wa miguu ya Pretoria Afrika Kusini relini , ilianza kutumia uwanja huo mnamo mwaka 1918, na tangu mwaka 1935 timu ya Berea Park FC imeshiriki kwenye kile kilichoitwa Ligi ya Soka ya Transvaal.
Moto
[hariri | hariri chanzo]Katika miaka ya 1990, jengo hilo lilitumika kwa ajili ya usimamizi na uwenyeji wa mikutano mbali mbali, lakini baadaye miundo ya uwanja ilianza kuharibika. Shule ya upili ya wasichana na wavulana pamoja ilitumia uwanja huo hadi tukio la moto mnamo Aprili mwaka 2010 uliofanya uharibifu mkubwa sana. Tangu wakati huo, tovuti na ardhi ya eneo hilo havijatumika tena kabisa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ cite web|url=http://www.espncricinfo.com/za/content/ground/59174.html |title=Berea Park | South Africa | Cricket Grounds |publisher=ESPN Cricinfo |date= |accessdate=2014-07-18
- ↑ cite web|url=http://www.espncricinfo.com/ci/content/story/60247.html Archived 17 Julai 2014 at the Wayback Machine. |title=| Cricket News | Global |publisher=ESPN Cricinfo |date= |accessdate=2014-07-18
- ↑ cite web |url=http://www.titans.co.za/history-of-titans-cricket.html |archive-url=https://web.archive.org/web/20140404211822/http://www.titans.co.za/history-of-titans-cricket.html |url-status=dead |archive-date=2014-04-04 |title=History of Titans Cricket |publisher=Titans.co.za |date=2014-07-10 |accessdate=2014-07-18
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Berea Park kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |