Belmopan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Belmopan
Nchi Belize
Mahali pa Belmopan nchini Belize

Belmopan ni mji mkuu wa Belize. Idadi ya wakazi ni takriban watu 15,000. Jina la mji liliundwa na maneno mawili ya "Belize" (=nchi) na "Mopan" ambayo ni mto wa karibu.

Belmopan iko kando ya mto Belize kwenye 17°15′N 88°46′W takriban mita 76 juu ya UB. Ilichukua nafasi ya Belize City mji mkuu wa awali ulioharibika kabisa na dhoruba ya tufani mwaka 1961. Mji ulipangwa kwa ajili ya wakazi 40,000 lakini haikukua ipasavyo.

Pamoja na ofisi za serikali na bunge kuna pia Chuo Kikuu cha Belize.

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Belmopan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.