Nenda kwa yaliyomo

Latitudo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka ′W)
Ramani ya dunia inayoonyesha mistari ya longitudo (toka juu kuelekea chini) na latitudo (toka kushoto kuelekea kulia).
Maelezo ya latitudo na longitudo.

Latitudo (kwa ing.: latitude) ni mahala pa mchoro wa dunia au ramani huonyesha kwa mistari iliolazwa ni njia ya kuonyesha mahali duniani kwa kutaja umbali wake kutoka ikweta kwa kipimo cha digrii (°).

Mahali penye ikweta kamili (kwa mfano Nanyuki katika Kenya) ina latitudo ya "0". Mahali pa mbali ni ncha ya kaskazini au ya kusini zinazotajwa kwa 90°. Pamoja na kipimo cha longitudo inataja mahali kamili duniani.

Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north) na "S" (south) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Digrii za latitudo hugawiwa katika umbali wa 60 dakika au minuti; dakika ya latitudo ni mita 1852 au maili moja ya kibahari. Dakika hugawiwa katika nukta au sekondi. Mfano: 13°19.717′ N.

Latitudo muhimu ni:

1. Ikweta (0°)

2. Tropiki ya kansa (23½°Kas)

3. Tropiki ya kaprikoni (23½°Kus)

4. Duara la aktiki (66½°Kas)

5. Duara la antaktika (66½°Kus)

Pamoja na namba ya longitudo inaonyesha mahali kamili kwenye uso wa dunia.